Zinazobamba

MAJANGA TENA CLOUDS TV NA REDIO, ITV,TCRA YAVIPIGA PINI,MSIGWA AIPONZA ITV,SOMA HAPO KUJUA



 
MAMLAKA ya Mawasiliano nchini (TCRA)imevipiga faini ya milioni 5  vituo vya utangazaji vya Clouds Redio na kituo  cha Independent Television (ITV ) huku pia ikipiga faini ya milioni 4 kituo cha Clouds Tv  pamoja kuvipa onyo kali  vituo hivyo,baada ya kukiuka kanuni za utangazaji .Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.

Akitoa hukumu hiyo leo Jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui wa (TCRA)Mapunda amesema vituo  vyote vimekiuka kanuni ya utangazaji ya mwaka 2005 baada ya kutenda makosa tofauti ambayo yenye lengo la kuipotosha jamii.

Mapunda amedai kuwa mnamo tarehe 9/05/2016 kituo cha Clouds  Redio katika kipindi cha Jahazi kilikiuka kanuni hizo baada ya mtangazaji wa kipindi hicho Eprahimu Kibonde  kushabikia  kijana mwenye umri wa miaka 14 ambaye alifanya mapenzi ya mbuzi.


Amesema katika kipindi hicho mtangazaji huyo alionekana kushabikia hali hiyo baada ya kusema Kijana aliyefanya mapenzi na mbuzi ilitakiwa atoe posa kwa mbuzi huyo, jambo ambalo linakwenda kinyume na sheria ya utangazaji ya mwaka 2005  Na.5(c),5(g),14(1).
Amesema baada ya kamati yake kubaini makosa hayo waliwasilina na uongozi wa Clouds media kutaka kupata utetezi wa kosa hilo lakini mmiliki wa Clouds redio Ruge Mtahaba ambapo katika maelezo yake ya awali alikili kosa kwa watangazaji hao kutozingatia sheria hiyo huku akiomba Mamlaka hiyo kuwasamehe.
Mbali na kipindi hicho pia Kamati hiyo imebaini ukiukwaji wa sheria hiyo kwenye kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa kila siku saa 12 asubuhi hadi saa 10 asubuhi ,amedai kuwa siku ya tarehe 18/5/2016  katika redio hiyo  watangazaji wa kipindi hicho walitumia maneno yasiyo na  staha.
Amedai kuwa katika kipindi hicho watangazaji hao walisoma taarifa kwenye magazeti inayosema “Mtoto wa miaka mitatu apandikishwa Uume” huku watangazaji hao wakiwasilisha taarifa hiyo kwa mzaha yenye kujaa kushabikia masuala ya ngono na kushindwa kusimamia kanuni za utangazaji.
Hata hivyo,amesema katika kipindi hicho kilikuwa hakina mtaalamu wa masula ya kitabibu wenye kutoa ukweli juu ya taarifa hiyo kutoka kwenye magazeti.
Mapunda amesema baada ya Mamlaka hiyo kubaini ukiukwaji huo wa kanuni waliwasiliana na Uongozi wa Redio hiyo ambapo utetezi wake  walisema watangazaji hao hawakufanya makosa kwani walitoa taarifa ilivyo kutoka kwenye magazeti.
Hata hivyo,Mapunda amesema utetezi wa Clouds Redio haukuwa na mshiko kwani watangazaji hao walishindwa kusimamia sheria ya utangazaji ya 2005 inayokataza kurusha maudhui yenye matusi kuanzia  saa 11.30 alfajili hadi saa 3 usiku kwani mda huo watoto wanakuwa macho.
  MAKOSA YA CLOUDS TV NA ITV.
Mapunda amesema mnamo tarehe 15/06/2016 kituo cha Independent television cha Dar es salaam(ITV) katika kipindi cha Kumekucha kilichorushwa hewani kati ya saa 1.00 asubuhi  na saa 1.30 asubuhi kilitangaza uchambuzi  wa Bajeti ya serikali ya mwaka 2016/2017 ambapo mtangazaji wa kipindi hicho,Godfrey Monyo  alifanya mahojiano na Mbunge wa Iringa Mjini,Peter Msigwa.
Amesema katika kipindi hicho Msigwa  alitamka kwamba Naibu Spika Dkt Tulia Akson kuwa anavaa “Pumpers” kwa ajili ya kujisaidia kwa  sababu amekuwa hawaachii watendaji wengine kiti na cha spika kwa ajili ya kuliongoza Bunge.
Mapunda amesema katika kipindi hicho mtangazaji alishindwa kuudhibiti mjadala huo jambo ambalo lilipeleka lugha za matusi kutoka.
Aidha,Mamlaka hiyo baada ya kubaini makosa hayo walifanya mawasiliano na Uongozi wa ITV,ambapo Mhariri wa kituo hicho,Steven Chuwa alitoa utetezi kuwa kipindi hicho kilikuwa live (moja kwa moja) kwahiyo ni vigumu mtangazaji  kuzuia hali hiyo pamoja na hata hadhi ya Mbunge Msigwa kwenye jamii kwani yeye mwenyewe angejua aina ya maneno kutamka.
Mapunda amesema baada ya utetezi huo,Mamlaka hiyo ikabaini kituo hicho kimekuka kanuni ya utangazaji ya mwaka 2005 inayokataza kituo kutoa maauzi yenye kugombanisha umoja na mshikamano na kutoa maneno yenye kuudhi Mamlaka za serikali.
  Katika hatua Nyengine TCRA imkipiga faini ya Milioni 4 kituo cha Clouds Television ambao inadaiwa mnamo tarehe 22/05/2016 katika kipindi cha “Hip Hop” kinachorushwa hewani saa 8.00 mchana hadi saa 12.00 jioni walirusha video ya “Thank for Coming” ya mwanamuziki F.A  pia katika kipindi hicho walirusha wimbo wa “Lil Bebbie” unaoitwa Break it Down ambapo katika nyimbo hizi  zilionyesha maudhui  ya baadhi ya wanawake wanaovaa nguo za uchi.
Amedai kuwa jambo la kuonyesha video hizo ni kinyume na sheria ya utangazaji ya mwaka 2005 inayokataza kuonyesha vipindi kama hivyo kwenye mda ambao watazamaji ni watoto.
Aidha,Mapunda amesema vituo vyote vilivyopewa adhabu hiyo watakiwa kulipa fedha hizo ndani ya siku 30 huku rufaa zikiwa wazi kwa kituo ambacho hakijalizika na hukumu hizo.