JAMES MBATIA AMRUSHA KOMBORA RAIS MAGUFULI,SOMA HAPO KUJUA
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia amesema
kitendo cha Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli kuendelea na mikutano
ya kisiasa mikoani na kuwazuia viongozi wa vyama vingine vya siasa ni kutaka
kukwamisha demokrasia nchini.
Akizungumza jana katika kipindi cha Funguka
kinachorushwa na Televisheni ya Azam, Mbatia alisema Rais Magufuli akiwa
Singida, aliviponda vyama vya upinzani kuwa vimekufa.
“Akiwa Singida Magufuli alisema vyama
vya siasa vya upinzani vimekufa na kuvilinganisha na nyoka aliyekanyagwa kichwa
na kubakiwa na mkia tu unaocheza cheza,” alisema.
Alisema Agosti 12, mwaka huu Magufuli alikuwa mtaa
wa Lumumba, jijini Dar es Salaam akizungumza na wanachama wake na
kuonyeshwa na televisheni mbalimbali akikijenga chama chake.
“Nani anakwenda kuweka rekodi vizuri
huko mikoani kwa anayoyasema Magufuli kama anazuia wapinzani wasifanye
siasa? Kwa hiyo yeye anajenga chama chake lakini anazuia wapinzani wasifanye
hivyo,”alisema.
Alisema ikumbukwe kuwa Tanzania ni ya watu wote na
wanatakiwa kufuata sheria na utaratibu uliowekwa na si vinginevyo.