POLISI WAENDELEA KUWAWEKEA VIZINGITI CHADEMA YAMKAMATA MFANYABIASHARA WA TISHERT,SOMA HAPO KUJUA
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema limejiandaa kudhibiti
maandamano ya Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania (Ukuta) yaliyoandaliwa na
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) yanayotarajiwa kufanyika Septemba
Mosi mwaka huu.
Wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini
Dar es Salaam, Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Simon
Sirro amewatoa hofu wakazi wa mkoa huo kuwa hakuna mtu na au kikundi chochote
cha watu kitakachofanya maandamano siku hiyo.
“Habari ya Ukuta haipo,umeshabomoka na
kama haujabomoka utabomoka, wakazi wa Dar es Salaam msiwe na hofu, fanyeni kazi
na hata siku hiyo hakuna mtu atakayejitokeza barabarani kuandamana,”amesema.
Kamanda Sirro amedai kuwa siasa zinatakiwa kufanywa
kwa amani na utulivu na kwamba wanasiasa wanaoitumia siasa kufanya vurugu
hawatafanikiwa.
“Mimi niwahakikishie kwamba tunajiandaa
kwelikweli kuhakikisha watu wanafuata sheria , anayetaka kuvunja sheria kwa
kufanya maandamano aanze yeye ili nasi tuanze naye,” amesema.
Ameongeza kuwa ” Suala la utii wa sheria ni
la msingi,kama kuna watu au kikundi cha watu kinataka kuitumia siasa kufanya
uvunjifu wa amani wajue kwamba nafasi hiyo kwa Dar es Salaam haipo.”
Aidha,Kamanda Sirro amesema August 20 2016 Jeshi la
Polisi lilipata taarifa toka kwa raia wema kuwa maeneo ya Kinondoni kuna duka
linauza flana zenye maneno ya uchochezi yaliyoandikwa ‘’TUJIPANGE
TUKATAE UDIKITETA UCHWARA’’ , ‘UKUTA’ ‘
Amesema Polisi baada ya kupata taarifa hizo walifika eneo la tukio na kumkamata mtuhumiwa aitwaye YORAM SETHY MBYELLAH miaka 42, mfanyabiashara na mkazi wa Mburahati akiwa anauza fulana hizo dukani kwake
Amesema Polisi baada ya kupata taarifa hizo walifika eneo la tukio na kumkamata mtuhumiwa aitwaye YORAM SETHY MBYELLAH miaka 42, mfanyabiashara na mkazi wa Mburahati akiwa anauza fulana hizo dukani kwake