TAARIFA MUHIMU KUHUSU AJIRA ZA WALIMU MWAKA HUU,SOMA HAPO KUJUA
Naibu Waziri ofisi ya Nchini,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi)Suleiman Jaffo (kulia)akizungumza na Mwandishi wa Fullhabari.blogs Karoli Vinsent (Kushoto) leo Jijini dar es Salaam |
Naibu waziri ofisi ya Nchi,Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (Tamisemi) Seleiman Jaffo
amewatoa hofu wahitimu wote nchini
waliosomea ualimu ambao wamekuwa wakisubili
ajira kutoka serikalini kwa muda mrefu,
Hivyo amewataka walimu hao kuwa na subira kwani
ajira hizo zitatangazwa mda wowote kutoka sasa.Anaandika KAROLI VINSENT endelea
nayo.
Jaffo ameitoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam
wakati alipokuwa akizungumza na Mtandao huu ambapo amesema wizara yake kwa
kushirikiana na wizara ya Elimu wameshamaliza hatua ya kwanza ya kuhakiki idadi haswa ya walimu wanaohitajika pamoja na ile idadi ya wahitimu wa masuala hayo .
Amesema zoezi lilobakia kwa sasa ni kumalizia
takwimu za walimu waliostaafu kazi pamoja na waliohama kutoka serikali kwenda
kwenye shule binafsi ili serikali iweze kujua idadi harisi ya pengo la walimu
nchini.
Hata hivyo,Jaffo amesema katika mwaka huu serikali
inampango wa kuongeza idadi ya ajira za walimu hadi kufikia walimu elfu 40000
katika ngazi za shule za msingi na sekondari.
Jaffo pia amesema kwa sasa ajira hizo zitapewa
kipaumbele katika maeneo ya pembezoni mwa nchi ambayo amedai kuwa kuna uhaba sana wa walimu .
Ameitaja mikoa hiyo ni Mkoa wa Kigoma,Mara,Tabora,Rukwa,kwa
mujibu wa Jaffo amewataka wahitimu hao kujiandaa kufundisha katika maeneo hayo na
kutoa dhana ya kufundisha kwenye shule za mijini.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni