REDIO ZAENDELEA KUFUNGWA ZANZIBAR,NI MUENDELEZO WA UBABE UBABE,SOMA HAPO KUJUA
![]() |
Mkurugenzi wa kituo cha radio cha Swahiba FM, Kassim Suleiman |
KADHIA ya
ufutwaji uchaguzi wa Zanzibar ikiwa haijapatiwa ufumbuzi, kumekuwa na hatua za
ukandamizaji wa uhuru wa habari hapa Zanzibar na tayari madhara yametokea. Anaandika Jabir Idrissa, Zanzibar … (endelea).
Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar ilichukua hatua katili tarehe 26 Oktoba 2015, ilipoamuru
kufungwa kwa kituo kipya cha redio cha Swahiba FM kwa maelezo kuwa kimevunja
sheria.
Mkurugenzi wa kituo
hicho, Kassim Suleiman ameiambia MwanaHALISI Online, kwamba kituo
hicho kilifungwa kwa uonevu kwa sababu “hata utaratibu wa kisheria
haukufuatwa.”
Kwa mujibu wa Sheria
ya Utangazaji ya Zanzibar, amesema hatua kama hiyo huchukuliwa baada ya mmiliki
wa kituo chenyewe kufahamishwa na kuwa amepewa nafasi rasmi ya kujitetea baada
ya kujulishwa kosa linalodaiwa kuwa limefanywa na kituo.
Kassim ambaye
aliwahi kuwa Naibu Mkurugenzi wa Sauti ya Tanzania Zanzibar (STZ) kabla ya
kubadilishwa na kuwa Shirika la Utangazaji la Zanzibar (ZBC), alisema
amelalamika rasmi kwa barua kwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar
(ZBC).
Kosa lililotajwa kuwa
kituo hicho kimefanya ni kutangaza tamko la Maalim Seif Shariff Hamad la Oktoba
26 la kwamba alikuwa anaonesha kuwa na kura nyingi na kutaka Tume ya Uchaguzi
itangaze matokeo bila ya kuchelewa.
Taarifa za ndani ya
Tume ya Utangazaji zinasema uamuzi huo wa kufunga kituo cha Swahiba FM,
kinachoendeshwa na kampuni inayomilikiwa na Chama cha Wananchi (CUF),
umechukuliwa bila ya Bodi ya Tume kujua.
Kisheria uamuzi wowote kama huo utachukuliwa baada ya Bodi
kujadili tuhuma na kutoa uamuzi wake. Mjumbe mmoja wa Bodi hiyo ameithibitishia
MwanaHALISI Online, kuwa hawakukaa kujadili suala hilo.
Juzi askari wa Jeshi la Polisi walivamia maeneo mbalimbali ya
mji wa Zanzibar na kukamata wauza magazeti, na kukamata wafanyakazi wa duka la
vitabu na machapisho la BMC kwa kuwa lilikuwa likitoa nakala za gazeti la
MwanaHALISI la Jumatatu baada ya gazeti hilo kutoonekana mitaani muda mfupi
lipobainika.
Habari hii kwahisani ya Mwanahalisi oline
No comments
Post a Comment