TAARIFA MUHIMU KUHUSU UKWELI WA AFYA YA MKAPA,SOMA HAPO KUJUA

MSEMAJI Mkuu wa
Serikali ya Tanzania, Assah Mwambene amekanusha taarifa zinazosambaa katika
mitandao ya kijamii kuhusu Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa kuwa amefariki Dunia. Anaandika Hamisi Mguta … (endelea).
Akizungunza
na waandishi wa habari katika ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es Salaam,
Mwambene amesema Rais Mkapa yupo salama na mzima wa afya na hakuna maradhi yoyote yanayomsumbua.
Mwambene amewaasa
watumiaji wa mitandao mbalimbali hasa Blogs kuacha kuitumia mitandao hiyo kwa
kupotosha umma na kuandika nambo yasiyo na ukweli ili kuepusha mifumuko ya
habari za upotishaji.
“Si jambo jema na
wanaofanya hivyo waache mara moja kabla ya hatua stahiki hazijachukuliwa,”
amesema Mwambene.
Amesema kuwa jambo la kumzushia mtu kifo si jambo zuri ambalo
amelizungumza kama ‘uchuro’ kwa mtu husika na kumtabiria mabaya.
“Mkapa yupo hai na
kesho pia atakuwepo katika sherehe za kumuapisha Rais mteule wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, John Magufuli,” amesema Mwmbene na kuongeza.
Serikali italishughulikia hili na tayari imeshaanza kukamata
baadhi ya watu mbalimbali ambao wanatoa taarifa za uongo zinazopelekea umma
kupotoka.
Amesema kuwa vyombo
vya habari vifanye kazi kwa uweredi ili kazi ya uandishi wao iwe ya usawa na kufuata
misingi ya uandishi, jambo ambalo wengi hukiuka kutokana kutofuata weredi wa
kazi zao
Habari hii kwanisani ya Mwanahalisi oline
No comments
Post a Comment