MSANII KALAPINA ACHARUKIA UBUNGE WAKE KINONDONI,AIBUKA NA KUSEMA KAHUJUMIWA,SOMA HAPO KUJUA
Aliyekuwa Mgombea wa Ubunge Jimbo la KinondoniKalama Masud(Kalapina)akizungumza na waandishi Habari leo jijini Dar es Salaa akipinga matokeo ya Ubunge |
ALIYEKUWA mgombea Mbunge katika Jimbo la Kinondoni
kwa Tiketi ya Chama cha ACT-Wazalendo,Kalama Masoud(Kalapina)ameibuka na
kuyapinga matokeo.Anaadika KAROLI VINSENT endelea nay.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Kalapina amesema
Matokeo yaliyompa ushindi mgombea wa chama cha wananchi CUF ambaye alikuwa
naungwa na vyama vinavyoundwa UKAWA,Abdul Mtulia yalikuwa yamesheneni dosari lukuki .
Amesema
katika kata 19 zilizopo katika Jimbo hilo matokeo yake hayakujumlishwa baada mawakala wake kudai walitishiwa na mawakala wa Ukawa na kulazimika kuacha kusimamia vituo hivo.
“ Yaani
mawakala wangu walitishwa na mawakala wa UKAWA,mapaka wakalazimika kuacha
kusimamia vituo, naamini kuondoka kwa
mawakala hawa ndio kura zangu za ubunge ndio zikikaibiwa,”
Wanahabari wakimsikiliza kwa makani msanii kalapina |
Ameyataja maeneo ambayo amedai mawakala wake
walitishiwa ni Kata ya kijitonyama,Tandale,ndugupi pamoja na Kigogo,
Hata
hivyo, Kalapina amesema baada ya kubaini kasoro hizo alilazimika kugomea
kusaini karatasi ya wagombea,
Pamoja
na hayo Kalapina amesema hatua iliyobaki sahivi kwake ni kwenda kufungua kesi
mahakamani ya kupinga matokeo hayo.
“Lazima niende mahakamani ambapo ndio sehemu pekee
ya kupata haki,kwahiyo jumatatu au jumanne ijayo nakwenda kufungua kesi
mahakamani ili nipate haki yangu ya msingi kwene jimbo langu la kinondoni.”
No comments
Post a Comment