DC MAKONDA AJA NA HICHI KINONDONI,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Mkuu wa wilaya ya Kinondoni DC Mkonda akizungumza na waandishi wa habari |
KATIKA
kuhakikisha suala la urasimu katika mahakama zilizopo wilaya ya kinondoni
linamalizika,mkuu wa wilaya hiyo Paul Makonda ameunda kamati ya maadili ya
mahakimu katika wilaya yake.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Jijini Dar Es salaam,Makonda amesema kamati hiyo itasaidia kuondoa kero wanazipata wakazi wa kinondoni kwenye mahakama za wilaya
yake.
Amesema mara
kwa mara kumekuwa na malamiko kutoka kwa wananch kuwa kumekuwa na ukimkwaji wa
haki ikiwemo Kutolewa lugha mbaya kutoka kwa Mahakimu na kucheleweshwa kwa makusudi hukumu za kesi,
Ambapo
amedai kuanzishwa kwa kamati hii itawasiadia wakazi wa kinondoni ambao
wanakumbana na matatizo hayo kufika kwenye ofisi ya yake na kukutana na Kamati
yake hiyo na kueleza kero hizo ambapo kamati hiyo itakuwa na jukumu la kutafuta
haki kwa wananchi.
Makonda
amewataja wajumbe wa kamati hiyo ni Paul
Mkonda,Celestine Onditi ambaye ni Katibu Tawala wilaya ya Kinondoni,Frank Mushi
Hakimu mkazi mfawidhi wilaya ya kinondoni,Devota Kisoka,Hakimu wa kisutu ambaye
mjumbe wa kuteuliwa na Jaji mkazi,
Wengine ni
Rose Kangwa aliyekuwa Jakimu Mkazi mahakama ya wilaya ya temeke ambaye
amehamishiwa kigoma,Dr Richard Kasungu mjumbe wa kuteuliwa
Hata
hivyo Makonda amesema Kamati hiyo itakuwa na majukumu ya kupokea malalamiko
yanayowasilishwa na wananchi kuhusu mahakama zote zilizopo wilayani hapo,
Pili,kufanya
uchunguzi wa maoni ya katika mwenendo wa mahakama.
No comments
Post a Comment