CUF YAUNGANA NA KAFULILA,YAAPA KUFIA MAHAKAMANI,NI KUPAMBANIA MAJIMBO SITA YALIYOFANYIWA HUJUMA NA CCM,SOMA HAPO KUJUA
![]() |
Aliyekuwa Mgombea Ubunge jimbo la Mbagara kwa tiketi ya CUF, Kondo Bungo |
VIONGOZI wa
Chama Wananchi (CUF), wamedhamiria kupinga matokeo ya ubunge katika majimbo
sita ambayo wamedai yameporwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), Anaandika Faki Sosi…(endelea).
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Ofisa Haki za Binaadamu na Sheria wa CUF, Mohamedi
Mluya amesema kuwa, jopo la wanasheria wa chama hicho wamejiandaa kufungua kesi
ya kupinga matokeo ya majimbo hayo wakidai walishinda.
Akitaja majimbo hayo
Mluya amesema kuwa ni Tabora Mjini, Newala, Pangani, Mtwara vijijini na Mbagala
ambapo kulikuwa na uvunjaji wa sheria ya uchaguzi.
Amesema kuwa
kasoro hizo ni matumizi ya fomu ambazo hazikujazwa kikamilifu, nyaraka
zinazoonesha idadi ya vituo vya kupiga kura na idadi ya watu waliojiandikisha
kupiga kura hazifanani pia hujuma za viongozi wa CCM, kuvamia vituo vya
majumisho kinyume na utaratibu nyakati za usiku wa manane.
“Sisi wanasheria wa
chama tunapinga matokeo hayo kutokana na kuwa uchaguzi wa kihuni ambapo maofisa
wa tume ya uchaguzi katika majimbo hayo wametumika na CCM, pia tunaamini katika
majimbo hayo sita tumeshinda,” amesema Mluya.
Aliyekuwa mgombea
ubunge wa Jimbo la Tabora Mjini, Mkufya Peter ambaye ni miongoni mwa wabunge
wanaopinga matokeo katika majimbo yao kutokana na alichodai kuwa ni kuporwa kwa
ushindi wake katika jimbo hilo amesema kuwa mgombea wa CCM aliyemtaja kwa jina
Emmanuel Mwakaseka, hakufanya kampeni kikamilifu kwa kutegemea kuiba kura.
“Tumeshuhudi kuwa
fomu namba 21b haikujazwa kikamilifu, kwa mfano wa
Kata ya Ndevelwa ambapo zilizotumika kama fomu halali za matokeo ilhali hazina
Jina la kituo cha kupiga kura, hazina majina ya mawakala, hapakuwa kuna sahihi
za wamakala hao pia fomu hizo zilikuwa hazina ‘serial number’ ambapo matokeo
yake yalikuwa yamembeba mgombea wa CCM,” amesema Peter.
Peter amesema kuwa,
suala la Katibu Mkuu wa CCM Wilaya ya Tabora kuingia katika kituo cha
majumuisho usiku wa manane kinyume na utaratibu kinaashiria wizi wa kura.
Mwenyekiti wa Vijana
CUF Taifa Hamidu Bobali ambaye ni Mbunge Mteule wa Jimbo la Mchinga ameitaka
mahakama kutenda haki kwa kuwaachia huru vijana waliokamatwa wakiwa wanasubiri
matokeo ya wagombea wao katika vituo ya majimbo mbalimbali.
Hivi karibuni gazeti hili liliripoti malalamiko ya mgombea wa
Jimbo la Mbagala, Kondo Bungo kuvurugwa kutokana na matokeo ya jimbo hilo
kubandikwa kinyemela na Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke ambaye alikuwa ni
msisimamizi mkuu wa jimbo.
Habari
hii kwahisani ya mwanahalisi oline
No comments
Post a Comment