KIKWETE AENDELEA KUMTEULIA WAKURUGENZI MAGUFULI,AMPA SHAVU PROFESA MBWETE,SOMA HAPO KUJUA

TAARIFA KWA
UMMA UTEUZI WA MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI WA KAMPUNI
YA SIMU TANZANIA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Prof. Tolly Salvatory Augustin Mbwette kuwa Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwa kipindi cha
miaka miaka mitatu kuanzia tarehe 12 Oktoba 2015.
Uteuzi huo ni kwa mujibu wa kifungu Na. 9 (4) (a) cha Sheria Na. 20 ya Mwaka 1993 iliyoanzisha Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). Prof. Tolly Salvatory Augustin Mbwette amekuwa Makamu Mkuu wa
Chuo Kikuu Huria Tanzania kwa kipindi cha miaka kumi kuanzia tarehe 13 Aprili
2005 hadi tarehe 13 Aprili 2015. Pia amekuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam, kwa taaluma ni Mhandisi ujenzi aliyobobea kwenye maeneo ya Mazingiria,
TEHAMA, Utawala na Menejimenti kwa zaidi ya miaka 25 na amesoma Vyuo Vikuu vya
Dar es Salaam, Tanzania; IHE Delft, Netherland; na Chuo Kikuu cha London,
Uingereza kwa ngazi ya Shahada ya Kwanza, Uzamili na Uzamivu. Pia ameshirikiana
na Vyuo Vikuu mbali mbali duniani kutoka Bara la Ulaya, Amerika, Asia na Afrika
katika maeneo ya uhandisi, utafiti, TEHAMA, uandishi wa vitabu na majarida
mbali mbali.
Imetolewa na:
KATIBU MKUU
Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia
No comments
Post a Comment