HATIMAYE SASA IDADI YA WABUNGE WA VITI MAALUM YATOKA RASMI,CCM,CHADEMA CUF WAAMBULIA HAWA,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
TUME ya Taifa uchaguzi nchini,NEC imetangaza idadi ya wabunge wa viti maalum ambapo vyama
vya Chama cha Mapinduzi CCM , chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema pamoja
na Chama cha Wananchi CUF vyote kwa pamoja vimepata wabunge baada ya kupata
angalau asilimia 5 ya kura halali za wabunge nchi nzima.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini dare s
Salaam,Mwenyekiti wa NEC,Jaji Damian Lubuva amesema Chama cha CCM kilipata
jumla ya kura milioni 8.3 na kufanikiwa kupata idadi ya wabunge 64 wakati chama
cha Chadema kimepata kura milioni 4.7 na kupata wabunge wa vita maalum 36,
Sanjari na vyama hivyo,Jaji Lubuva pia amekitaja
chama kingine kilichopata wabunge wa viti maalum ni chama cha Wananchi CUF
kimepata kura milioni 1.2 na kufanikiwa
kupata wabunge wa viti maalum 10.
Hata hivyo jaji Lubuva ameainisha kuwa idadi ya
wabunge wa viti maalum ilitakiwa kuwa ni 113 lakini kwa sasa wamegawa wabunge
110 huku wabunge watatu waliobakia watapatikana baada ya kumalizika kwa majimbo
tisa ya ubunge ambayo hayajafanya uchaguzi,
Pamoja na hayo amebainisha kuwa Majina ya wabunge
husika ya Viti maalum yatatolewa na vyma husika baada ya tume kuhakiki majini
hayo na teyari wameyarudisha kwenye vyama husika
Hakuna maoni
Chapisha Maoni