Zinazobamba

POLISI WAENDELEA KUISAKAMA CHADEMA NA UKAWA,WAIPIGA TENA MARUFUKU MKUTANO WAKE WA NCHI NZIMA JUMAPILI,SOMA HAPO KUJUA

Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (SSP), Advera BulimbaPOL

JESHI la Polisi nchini limepiga marufuku mikutano yote ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema  iliyotarajiwa kufanyika kesho kutwa Jumapili nchi nzima.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo
    Akitoa katazo hilo, leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na waandishi wa habari  na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini,Advera Bulimba  ambapo amesema Jeshi la Polisi limepata barua kutoka kwa Chadema iliyokuwa inataka kuomba ruhusa ya kufanyika kwa mkutano kila mkoa ambao ulitakiwa kufanyika jumapili wenye lengo la kutoa sera kwa wananchama wake.
     Bulimba amesema mara baada ya Jeshi hilo kupata barua hiyo wakafanya Tasmini na kubaini bado nchini kuhali tata ya usalama.
“Tumekata mikutano hii,baada ya kubaini kuna mihemuko ya kisiasa ndani ya jamii yetu,hivyo  mikutano au maandamano ya aina hiyo inaweza kusababisha uvunjifu wa amani  endapo ikutuhusiwa”amesema Bulimba.
Ameongeza kuwa “Jeshi la Polisi bado linasisitiza katazo lake la awali  liliozuia mikutano na maandamano mpaka hapo hali itakapotengamaa”

Hata hivyo,Jeshi hilo la Polisi nchini linatoa wito kwa wananchi wote nchini kuendelea kutoa ushirikiano katika kipindi chote cha uchaguzi kwa kujiepusha na vitendo vyovyote vitavyoleta uvunjifu wa amani

Hakuna maoni