KAMATI KUU YA CHADEMA YATOA MAAMUZI MAZITO,SOMA HAPA KUJUA

KAMATI Kuu ya Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), imeazimia na kulaani tabia ya Rais Jakaya
Kikwete kusafiri ovyo nje ya nchi wakati taifa lipo katika kipindi kigumu na
matatizo makubwa ambayo yanahitaji uongozi thabiti. Anaandika
Sarafina Lidwino…(endelea.)
Kamati
Kuu ilikutana kwa siku mbili kati ya tarehe 3 hadi 5 Mei mwaka huu, na kuitaka
pia serikali kuchukua hatua za dharura kunusuru shilingi kwani athari zake ni
kubwa sana kiuchumi na kijamii na kwamba zitasababisha mfumuko wa bei.
Akisoma
maazimio hayo leo kwa waandishi wa habari katika Makao Makuu ya Chadema
yaliyopo mtaa wa Ufipa Kinondoni, Katibu Mkuu wake, Dk. Willibrod Slaa, amesema
kamati kuu vile vile ilipokea na kujadili hali halisi ya sekta ya usafirishaji
nchini.
Amesema
kuwa, wamebaini udhaifu mkubwa ambao upo ndani ya sekta hiyo kutokana na
usimamizi dhaifu wa watu ambao walipewa dhamana kuanzia Waziri wa Uchukuzi,
Samuel Sitta ambaye ameshindwa kabisa.
“Hali hiyo inasababisha sekta hiyo
kukosa mwelekeo na hivyo kuleta madhara mengi kwa wananchi kutokana na ajali za
kila siku kuanzia vyombo vya majini na barabarani. Kamati kuu imebaini kutokana
na mgomo wa madereva wananchi wameathirika kisaikolojia na kiuchumi,”amesema.
Kwa mujibu wa Dk. Slaa, Kamati kuu, imeazimia kuunga mkono madai ya
madereva kwani ni halali na hivyo ni lazima serikali iyatekeleze madai yao yote
ya muda mrefu. Amesema “kuendelea kuyapuuza ni kukubali kuendelea kuhatarisha
maisha ya abiria.”
Kuhusu
uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu, Dk. Slaa amesema kamati kuu imepokea taarifa
ya kina namna ambavyo hadi sasa maandalizi ya msingi kisheria hayajafanyika.
Ametaja kuwa ni mandalizi ya vifaa, fedha, kutangaza majimbo na kata mpya,
kutangaza vituo na kusuasua kwa uandikishaji wapiga kura.
“Katika jambo hili, kamati kuu imeazimia kuwa uchaguzi huo lazima
ufanyike Oktoba kwa mujibu wa Katiba na serikali ya CCM isijiandae kutumia
kisingizio chochote kuahirisha kwa sababu uchaguzi sio jambo la dharura, bali
lilijulikana miaka mitano iliyopita,” amefafanua.
Chanzo ni Mwanahalisi.oline
No comments
Post a Comment