HABARI KUBWA LEO-CHADEMA YAFUNGUA MILANGO YAKE SASA,SOMA HAPA KUJUA

HATIMAYE Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimefungua
milango kwa wanachama wake wenye sifa za uongozi kuchukua fomu za kuomba
kuteuliwa kugombea wa udiwani, ubunge na urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka
huu.Anaandika
Sarafina Lidwino…(endelea).
Akizungumza na waandishi wa habari leo,
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa amesema, mwanachama aliye tayari
ajitokeze kuchukua fomu hizo.
Kwa kuzingatia makubaliano ya
ushirikiano wao na vyama vinavyounda kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa) vya CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, ratiba ya Chadema imejikita zaidi katika
kata na majimbo ambayo hawana wawakilishi.
Dk. Slaa amesema kuwa Mei 18 hadi Juni
6 mwaka huu, wanachama watachukua na kurejesha fomu za udiwani katika kata
ambazo hawana madiwani kutoka kwa makatibu kata/ jimbo na wilaya.
Julai mosi hadi 10, watachukua na kurejesha
fomu wagombea katika kata ambazo kuna madiwani wa Chadema na kati ya Julai 15
hadi 20 itakuwa ni uteuzi wa mwisho wagombea udiwani wa kata pamoja na wale wa
Viti maalumu chini ya kamati tendaji za majimbo.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, Mei
18 hadi 25, watachukua fomu wagombea ubunge katika majimbo ambayo Chadme haina
wabunge kwa sasa, pamoja na fomu za ubunge wa viti maalum kutoka kwa makatibu
wa majimbo, wilaya, mikoa,mikoa na makao makuu.
Julai 6 hadi 10, watachukua na
kurejesha fomu za ubunge wagombe katika majimbo ambayo yana wabunge wa Chadema
kwa sasa huku Julai 20 hadi 25, itakuwa uteuzi wa awali kwa wagombe hao.
Dk. Slaa ameongeza kuwa
kuanzia tarehe hiyo ya Julai 20 hadi 25, milango ya wanachama wa Chadema
wanaotaka kuwania kiti cha urais itafunguliwa rasmi makao makuu, huku uteuzi wa
mwisho wa wagombea ubunge ukifanyika kati ya Agosti mosi hadi 8 mwaka huu
chini ya Kamati Kuu.
“Tarehe 3 Agosti Baraza Kuu
Taifa litakutana na Mkutano Mkuu utafanyika siku inayofuata, lakini uteuzi wa
mgombea wetu wa urais utazingatia makubaliano ya Ukawa,” amesema Dk. Slaa
Chanzo ni Mwanahalisi.oline
No comments
Post a Comment