Zinazobamba

DC MAKONDA AZIDI WALILIA MADEREVA TIZAMA ALICHOSEMA LEO KWA KUBOFYA HAPO

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza na wandishi wa habari hawapo pichani  ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.

Madereva wamepewa kipaumbele  kwenye tume itakayokuwaikisimamia usafirishaji,kwani tume hiyo itakuwa na wajumbe watano  kutoka  Umoja wa madereva tuu na kutoka sekta nyingine watakuwa wajumbe watatu Anaandika Avila Kakingo,Globu ya Jamii endelea nayo .
         Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda  wakati akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake  jijini Dar es Salaam leo.

       Makonda amesema kuwa kamati hiyo haitaundwa na serikali, wajumbe watatokana na  uchaguzi wa madereva wenyewe pia  na wajumbe wengine watatoka  Mamlaka ya usafirishaji (SUMATRA), TABOA , TATOA, Wizara ya Ajira, wizara ya na mambo ya ndani.

          Makonda ameongezea kuwa Mgomo wa madereva hautakuwepo tena milele, madereva wachague wajumbe  ambao wanaweza kuhakikisha haki zao kinasimamiwa vizuri na kutatua matatizo yao.

Chanzo ni Michuzi.blogs

No comments