Zinazobamba

HABARI KUBWA LEO,JIJI LA DAR LIMEHARIBIKA LOTE,SERIKALI YAWARUKA WATU WA MABONDENI YASEMA KAMA WAFE WAFE TU SOMA HAPO







MAFURIKO,Mafuriko,Mafuriko .! Jiji
la Dar limejaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha wengine kukosa makazi.

       Maeneo yaliyokumbwa kwa mafuriko ni Mnyamani
(Ilala),Bonde la Mpunga (Kinondoni) ,Kigogo (Kinondoni),Mikocheni ( Kinondoni),Vingunguti (Ilala) Tabata Kisiwani (Ilala)na Kurasini (Temeke) na maeneo mengine ambayo hayajawahi kupata mafuriko yamefika.

           Mvua hizo zimeharibu miundombinu katika
barabara ya Morogoro kwa kujaa maji na kufanya kutokuwepo kwa usafiri kuelekea katikati ya
jiji la Dar es Salaam.


        Wilaya ya Kinondoni ndio inaongoza kwa maeneo
mengi kukumbwa na mafuriko kutokana na watu kujenga katika mikondo ya maji na
baadhi ya watu kujenga nyumba katika miundombinu ya maji mitalo ya  maji
taka na  kufanya maeneo mengine kutapakaa maji na kuleta adha ya usafiri.


        Kwa Wilaya Ilala ni eneo moja ndilo limekuwa
likisababisha mafuriko, ni kwa wale waliojenga karibu na bonde la mto Msimbazi  ndio wamekuwa waathirika wa mafuriko kila mwaka
     Wananchi wa maeneo yaliyokumbwa na mafuriko
hawana msaada wowote huku mvua ikiendelea kunyesha kuanzia majira ya saa 10
jioni na kuamkia leo hadi katika muda huu mvua inatikisa.






       Akizungumza na Ripota wa Globu ya Jamii,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadick amesema kuwa serikali msaada wake ni
wale waliopata madhara kutokana na mvua hizo na sio kuwapa makazi na chakula kutokana na kukataa kuhama maeneo hayo na kuishia kuipeleka serikali
mahakamani.





          Mkuu wa Mkoa amesema serikali ilitoa maeneo
mbadala ya kwenda kujenga na kuishi kwa watu wa maeneo ambayo mara kwa mara
wamekuwa wakipata mafuriko, walikataa na kuipeleka serikali mahakamani hivyo sasa haiwezi kuwasaidia.






         “Sasa sisi tufanye nini tutawaombea sala,lakini msaada kwetu ni wale waliopata madhara ya kiafya kwa ajili
matibabu,Serikali ndio itafanya hivyo”amesema Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.


        Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum
ya Dar es Salaam,Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP),Suleiman Kova amesema katika
mvua zinazoendelea mtu mmoja amepoteza maisha kwa kuanguka katika mto ng’ombe uliyopo eneo la Mburahati jijini Dar es Salaam.


      Kamanda Kova amesema aliyepoteza maisha ni
Shaban Idd (73) Mkazi wa Manzese jijini Dar es Salaam na mwili wake umeopolewa
na kuhifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala.

No comments