HABARI ILIYOTIKISA NCHI-LOWASSA AVUNJA UKIMYA,NA AMWAGA MANYANGA RASMI,SOMA CHOTE ALICHOKISEMA HAPO
![]() |
Pichani ni Edward Lowassa |
BAADA ya
Kimya kizito hatimaye Edward lowassa, naweza kusema ameamua kuvunja ukimya huo
na kuibuka kutamka wazi wazi kwamba anaitaka Nafasi ya Urais ndani Chama cha
Mapinduzi CCM kwenye Uchaguzi Mkuu wa hapo baadae mwaka huu .Anaripoti KAROLI
VINSENT endelea nayo.
Kuibuka kwa Lowassa ambaye ni Waziri
mkuu aliyejiuzulu kwa Kashfa ya Ufisadi kwenye Kampuni Tata ya Richmound ,kuna kuja siku moja kupita
baada CCM kutangaza rasmi tarehe kwa makada wake kuanza kuchukua Fomu ya
kuwania kwenye uongozi mbali mbali kwenye Uchaguzi mkuu hapo baadae .
Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli
CCM ameisema kauli hiyo leo Nyumbani kwako Mkoani Dodoma wakati alipokuwa akizungumza na Wahariri mbali mbali wa Habari ambapo
amesema yupo Vizuti katika kuwania nafasi ya Urais na anatarajia kutangaza
rasmi hapo Jumamosi ya wiki hii.
“Nataka kuwahakikishia nyinyi na watanzania
niko vizuri kwa teyari kwa chochote na nipo sawa kuwania nafasi ya Urais ambayo
natarajia kutangaza hapo Jumamosi”amesema Lowassa.
Lowassa ambaye pia ni Mwenyikiti wa
Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano kimataifa amesema kutokana na
tatizo la kubwa la Vijana kukosa Ajira ndio miongoni mwa sababu iliomfanya
ajitose kwenye Nafasi hiyo kubwa na uongozi wanchi.
“Tatizo la
Ajira ni Bomu ambalo linatarajia kuripuka na,kwakuwa wako vijana wengi wamemaliza Vyuo vikuu hawana
Ajira wapo mitaani unategemea nini,wakati wenzetu katika nchi zilizoendelea
katika kipindi cha Kampeni wanaweka wazi mambo ya Ajira, na sio kuwekeza kwenye
Kilimo Kwanza na hata chama changu wanajua kwamba sera ya Kilimo kwanza
siikubaliani nayo unaitaji taifa liloendelea kwa kuwekeza kwenye Elimu.”
KUHUSU AFYA YAKE
Lowasa
amesema kuhusu suala la Afya ni amedai ni chuki tu ipo kwenye Chama chake cha CCM.
“Kuna chuki
imeingia ndani ya chama chetu na mimi nasema chama chetu waweke utaratibu wa
kupima Afya ambao tunagombania nafasi ya Urais
waweke utaratibu wa kufanya hivyo na mimi nawahakikishia nipo vizuri”amesema
Lowassa.
KUHUSU KUHAMA CCM.
Lowassa pia
alizungumzia suala hilo ambalo mara kwa mara lilikuwa likiandikwa kwenye
magazeti ambayo yalikuwa yakidai endepo atakatwa jina lake ndani ya CCM
atajiunga kwenye Chama kipya cha kisiasa cha ACT-Wazaendo.
Ambapo
lowassa amesema hawezi kuhama chama hicho kikongwe kilichopo barani Afrika.
“Kuhama chama sina mpango nimeamia
CCM mwaka 1977 sijafanya kazi sehemu popote zaidi ya CCM maisha yangu yote yapo
CCM anayetaka nihame basi ahame yeye”.
VIJEMBE KWA UTAWALA WA KIKWETE.
Sanjari na
kuweka mipango ya kuwaokoa Vijana pia Mwanasiasa huyo Mkongwe akusita kutoa
Vijembe kwa Rais anayemaliza mda wake Rais Jakaya kikwete kwa kusema limefika
hapo kwenye matatizo kutokana na kuwa kwa watendaji wabovu wanaofanya kazi
kimazoea.
KUHUSU MADAI ANAYODAI NI YA VISASI.
Lowassa
ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM amesema kuhusu Visasi kwamba
yeye ni ni Mkristo na hana Visasi na mtu yeyote.
“Mimi ni
Mkristo hata bwana yesu alisema samehe mara sabini sina kisasi na mtu yeyote”
KUHUSU HALI YA UPINZANI.
Mbali na
mambo hayo pia Lowassa amezungumzia hali ya vyama vya Upinzani na ameikitaka chama
chake kisizubae.
“Nachoweza
kusema kwamba Upinzani umepata nguvu,mijini na Vijijini, sisi ni chama
kinachoshika Dola tusizubae na wenzetu wameanza pata nguvu tusibweteke,maana
wenzetu wamejiandaa vizuri,na sisi tunapaswa kujipanga maana Vyama vya Ukombozi
Afrika vimeondolewa kwahiyo tusijisahu maana ukitoka madakani urudi”
Post Comment
Hakuna maoni
Chapisha Maoni