KUBWA LEO-KUMEKUCHA UCHAGUZI MKUU,NEC YAIBUKA YATAJA TAREHE YAKE,NI BAADA YA KILIO CHA MBOWE,SOMA HAPO KUJUA

SIKU moja kupita baada ya chama cha Mapinduzi CCM kufungua Milango kwa Wanachama wake kuanza kuchukua Fomu za kuwania Uongozi kwenye Uchaguzi mkuu,nao pia Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini (NEC) imetangaza Rasmi tarehe ya Uchaguzi Mkuu, siku ya uteuzi wa Wagombe pamoja na siku ya kuanza kampeni za Uchaguzi mkuu.Anaripoti KAROLI VINSENT endelea nayo
Kwa Mujibu wa Taarifa ya NEC kwa Vyombo
vya Habari nchini iliyosainiwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Damiani
Lubuva ambapo inasema kuwa kwa Mujibu wa vifungu vya Katiba ya nchi ni cha 35 B (1),(3)(a),37 (1) (a)
na 46 (1),sura ya 343, inatoa Mamlaka
NEC kutangaza Ratiba hiyo.
Pamoja na hayo amebainisha kuwa siku
ya Uteuzi wa Wagombea Urais,Ubunge na
Udiwani utafanyika tarehe 21 Agosti
mwaka huu,
Sanjari na
hayo pia Kampeni za Uchaguzi nazo zitaanza tarehe 22Agosti mpaka tarehe 24
Octoba mwaka huu,
Ambapo Siku
ya kupiga kura nchi nzima itafanyika tarehe 25 Oktoba mwaka huu.
Kuibuka huko kwa NEC katika kutoa
Ratiba ya Uchaguzi kunakuja Siku Moja kupita baada ya Mwenyekiti wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman Mbowe kumtaka Jaji Lubuva kuweka bayana
utaratibu wa Uchaguzi ikiwemo siku ya Kampeni pamoja na Tarehe ya kupiga kura.
Post Comment
Hakuna maoni
Chapisha Maoni