Zinazobamba

WWF YAZINDUA MPANGO WA KUSHIRIKISHA VIJANA KWENYE MAZINGIRA.

*Yawasihi Vijana kutunza Mazingira kulisaidia Taifa.

*Vijana wafurahishwa na mpango huo,waapa kuwa mabalozi wa Mazingira 

Na Mussa Augustine.

Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa
Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira la WWF, Yohana Mpagama,amewasihi Vijana kutunza Mazingira ili kulisaidia Taifa kukabiliana na majanga yanayoweza kutokana na mabadiliko ya Tabianchi.

Mpagama ametoa wito huo leo Machi 14,2025 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa mpango wa kushirikisha vijana kwenye Mazingira(WWF YOUTH INTAVION CHAMPION) nakusema kuwa vijana ni nguvu kazi ya Taifa na wanahitajika katika kulinda mazingira.

"Napenda kutoa  rai kwa vijana watambue kuwa sio nguvu kazi ya kesho tu,bali ni nguvu kazi ya leo,hivyo mnapaswa kutambua wajibu wenu kama Mabalozi wa uhifadhi wa mazingira ili kutimiza malengo yetu ya kuwa na Dunia yenye Mazingira salama."amesema

Nakuongeza kuwa "shirika la WWF litaendelea kuwasapoti Vijana katika kutunza mazingira na kusaidia kuondoka na na athari zinazotokana na Mabadiliko ya Tabianchi ambayo yamekua yakisababisha athari kubwa ikiwemo ukame.

Nae Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano WWF Tanzania,Joan Itanisa,amesema mpango huo wa kuwashirikisha vijana kwenye mazingira umewashirikisha vijana kutoka sehemu mbalimbali nchini kwa lengo la kufikisha ujumbe kwenye maeneo wanayotoka ili kuhamasisha vijana wenzao kushiriki katika kuhifadhi mazingira.

"Vijana hawashiriki kikamilifu katika kuhifadhi mazingira kwa kuona hakuna faida kwao na wengi kujikita katika shughuli za kujitafutia Kipato,hivyo tumeona tuwashirikishe ili waweze kuwa mabalozi Wazuri wa Mazingira". amesisitiza Joan.

Joan ameongeza kuwa uelewa mdogo wa Vijana kuhusu uhifadhi wa Mazingira umekua  kikwazo kwa vijana hao kushiriki kikamilifu katika uhifadhi wa Mazingira ,nakwamba  WWF itaendelea kutoa elimu kwa vijana kuhusu uhifadhi wa Mazingira.

Hata hivyo baadhi ya vijana walioshiriki mafunzo hayo ya siku mbili akiwemo Joseph Magele kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi ,amesema mpango huo umewajenga vizuri ambapo wao watakua mabalozi wazuri katika utunzaji wa  mazingira Nchini.

"Kwa sasa kumekua na  ongezeko la joto,hali hii inatokana  na shughuli za kibinadamu,ikiwemo ukataji holela wa miti,sisi kama Vijana tunapaswa kutoa Elimu kwa jamii ili itambue umuhimu wa kutunza Mazingira na kuepukana na athari mbalimbali." amesema Magele

Nakuongeza kuwa" WWF imeleta mpango mzuri sana wa kushirikisha Vijana kwa kuwapatia elimu ya utunzaji wa Mazingira,hivyo tutakua mabalozi wazuri katika kulisaidia Taifa letu kuondokana na mabadiliko ya Tabianchi".

Hakuna maoni