DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA ZANZIBAR LAHITIMISHWA LEO WILAYA YA KATI,KESHO WILAYA YA KUSINI UNGUJA
Mwandishi Wetu Zanzibar
Daftari la Kudumu la Wapiga kura Zanzibar linahitimishwa leo wilaya ya kati na kesho linaanza wilaya ya Kusini, Unguja.
Akizungumza na Afrika Leo, Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis alisema daftari hilo linaingia mkoa huo baada ya kutamatika katika Mkoa wa Mjini Magharibi.
Mwenezi Mbeto alisema kulingana na ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), daftari jana 8 Machi 2025 limeanzia wilaya ya Kusini na uandikishaji unaendelea vizuri.
"Wameanza jana na mchakato unaendelea vizuri" alisema na kuongeza kuwa wakimaliza wataingia wilaya ya Kati.
Alibainisha kuwa daftari hilo lililoanzia visiwani Pemba, litamalizia wilaya ya Mjini Machi 15 mwaka huu na amehimiza wananchi kujitokeza kujiandikishaa.
Daftari hilo ambalo linaandikisha wapiga kura wapya wenye sifa na wengine kurekebisha taarifa zao ni sehemu ya safari ya kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025.
Kulingana na ZEC wanaostahili kuandikishwa ni wote wenye sifa ya ukaazi wa Zanzibar.
Sheria Namba 4 ya Mwaka 2018 imetaja wenye sifa
Post Comment
Hakuna maoni
Chapisha Maoni