HOT NEWS-LOWASSA AANZA VITA NA KIKWETE,SASA NI KISASI NA VISASI,SOMA HAPO KUJUA
![]() |
PICHANI NI EDWARD LOWASSA |
WAZIRI Mkuu
aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond mwaka 2008, Edward Lowassa ameanza safari
ya kujiimarisha kisiasa kuelekea mbio za urais kupitia Chama Cha Mapinduzi
(CCM), akiwashambulia waziwazi viongozi wenzake, akiwemo Mwenyekiti, Jakaya
Kikwete…Anaandika Mwandishi Wetu …(endelea).
Lowassa
ambaye alikuwa msaidizi wa Rais Kikwete kwa miaka miwili kama msimamizi wa
shughuli za Serikali, amepingana na bosi wake akisema alikosea kuanza na kilimo
kwanza na kuweka elimu kando.
Kauli ya Lowassa inakinzana na
utaratibu wa CCM unaowataka viongozi kupingana au kukosoana kupitia vikao
badala ya kufanya hivyo hadharani, hatua inayotafsiriwa kama kudhoofisha chama.
Badala yake, Lowassa ametamba kuwa, akiwa
rais ataanza kushughulika na elimu kama lengo kubwa na sio kilimo kwanza cha
serikali ya Kikwete.
Vigogo wengine wa CCM aliowashambulia ni
aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa, Samuel Sitta na Dk. Harrison Mwakyembe,
aliyeongoza Kamati teule, akisema wawili hao walipika ripoti ya kashfa hiyo ili
kumdhalilisha.
Lowassa na makada
wenzake watano, Fredrick Sumaye, Steven Wassira, Bernard Membe, January Makamba
na William Ngeleja, waliondolewa kifungoni Mei 23 mwaka huu, baada ya kufungiwa
kwa mwaka mmoja kwa tuhuma za kuanza mchakato mapema ndani ya chama.
Katika kile kilichoonekana kama kujibu
mapigo ya tuhuma za ufisadi dhidi yake, Lowassa aliwaalika baadhi ya wahariri
wachache kutoka Jukwaa la Wahariri nyumbani kwake mjini Dodoma leo, na
kufafanua baadhi ya mambo kadhaa kupitia “wateule wake” hao.
Akizungumzia tuhuma za zabuni tata ya
Richmond Development LLC, Lowassa amesema “sihusiki na lolote kuhusu sakata
hilo na ndio sababu hata Kamati ya Mwakyembe haikunihoji.”
Amesisitiza kuwa, cheo cha uwaziri mkuu
ndicho kilikuwa lengo la kamati ya Dk. Mwakyembe na Spika Sitta kumshughulikia.
“Hicho sio kikwazo kwangu katika
kuingia Ikulu, kwani sakata la Richmond lilipikwa kunichafua. Nimechukua muda
mrefu kuzungumzia hili la Richmond na nitalisema zaidi Arusha wikendi hii,”
amesema Lowassa ambaye atatangaza nia ya kuwania urais siku hiyo.
Kuhusu kutumia makundi
ya kumshawishi kutangaza nia, Lowassa
amesema “naamini kila mtangaza nia ana makundi ya kumuunga mkono.”
Mkutano wake huo, mbali na wahariri pia
ulihudhuriwa na Nazir Karamagi-mmoja wa mawaziri waliojiuzulu pamoja na Lowassa
mwaka 2008 kwa kashfa hiyo, wabunge Peter Serukamba, Diana Chilolo.
Walikuwepo pia wafuasi
wake wengine, Hussein Bashe, baadhi ya waliokuwa wakuu wa wilaya walioenguliwa
kama Elibariki Kingu (Igunga) na aliyekuwa Mkurugenzi wa HakiElimu, Elizabeti
Misoki.
Misoki ametangazwa rasmi kuwa
mkurugenzi wa mahusiano na mawasiliano katika timu ya kampeni ya Lowassa.
Amehoji kwani akina Karamagi wana tatizo gani na kwani wao sio binadamu?
Kuhusu mabilioni ya fedha anazogawa kwa
baadhi ya makundi, Lowassa anasema anapata michango ya rafiki zake na kwamba
ataendelea kupokea michango hiyo wakati wote wa harakati zake na haina madhara
yotote.
“Sitahama CCM. Asiyenitaka ndiye
aondoke kwenye chama kwani mimi nina uhakika wa kupata nafasi ya kuwania
urais,” amesema.
Lowassa amefafanua kuwa, hatalipa
kisasi kwa lolote lililomtokea katika siasa kwani, amemwachia Mungu kwa vile
yeye ni mcha Mungu.
Ametamba kuwa Arusha itawaka moto tarehe
30 mwezi huu, na kuwataka Watanzania kutega sikio kwani ataanika kila jambo
kuhusu mustakabali wa nchi hii na mipango yake ya kuiinua nchi kiuchumi katika
miaka kumi ijayo.
Chanzo ni Mwanahalisi oline
Post Comment
Hakuna maoni
Chapisha Maoni