WACHIMBA MADINI WADOGOWADOGO WAMWAGA CHOZI KWA KAMISHINA WA MADINI
Kamishan wa Madini Nchini Hamis Komba akitazama bidhaa ndogondogo za Madini zilizotengenezwa na wachimbaji wadogowadogo |
Wachimbaji wa madini wazalendo toka mikoa mbalimbali leo hii wametoa kilio chao juu ya matatizo mbalimbali yanayowakabili kwa kamishina wa madini ili waweze kusaidiwa,
Akizungumza na waandishi wa habari,Mwenyekiti wa chama cha wachimba madini wanawake (TAWOMA) Bi. Ubice Negele Amesema wanachama wake toka mikoa mbalimbali wanakabiliwa na tatizo kubwa la kupata elimu juu ya uwelewa wa thamani ya madini,madni yenyewe na ufundi wa kukata madini hayo ili kuyaongezea thamani.
Bi. Unice amesema wachimbaji wadogowadogo wamekuwa na wakati mgumu sana katika kutambua thamani halisi ya madini na hivyo kushindwa kuuza madini hayo kwa bei stahili
Akijibu, Vilio vyao,kamishina wa madini toka wizarani Bw.Hamisi Komba amesema matatizo hayo ni sugu lakini anayachukua ili kuweza kuyafanyia kazi ili kutatua kero hiyo inayowakabili
Tumesikia juu ya kilio hangu,hapa nimekuja na msaidizi wangu Bi. Teresia nafahamu atayachukua na kuyafikisha ofisini ili tuyafanyie kazi ili tuweze kuyaweka mazingira mazuri ya biashara ya madini,
Akifungua warsha hiyo Mwenyekiti wa TAWOMA Taifa Eunice Negela alisema kuwa wameaanda
warsha hiyo wakishirikiana na Wizara ya Nishati na Madini wakiwa na mkakati wa
kumkomboa,kumuinua na kumuelimisha wanawake wadogo wachimba madini.
Alisema kuwa chama chao kina wanachama 500 nchi nzima lakini katika warsha hiyo wamefikala
wawakilishi kutoka mikoa mbalimbali nchi nzima ilikuwakutanisha kwa pamoja na kubadilisha
uzoefu juu ya uchimbaji madini.
"Tunahitaji mafunzo ya uchimabji ili tupate ufanisi zaidi wa kujua utambuzi wa madini
pamoja na thamani pia tupate maarifa katika masuala ya sheria, biashara na utafutaji wa
masoko kwani wengi wetu hatuna elimu ya kutosha ya masuala haya "alisema Negela
Aliongeza kuwa changamoto kubwa zinazo wakabili ni upatikanaji wa soko huru la pamoja
ambapo wachimbaji wote wataweza kuweka na kunadi bidhaa zao bila ya bugudha ya kupangiwa
bei au kuibiwa.
alisema kuwa kazi ya kumuinua mchimbaji mdogo hasa mwananmke ni ngumu kutokana na ukosefu
wa soko huru ambalo lingewasaidia kwani wachimbaji wengi wamekuwa wakidhulumiwa kwasababu
wengi wao hawajui bei halali na thamani ya madini walionayo.
"serikali kupitia wizara ya nishati na madini imekua mstari wa mbele kuwainua wachimbaji
hawa ambapo tayari wameaanza kutoa ruzuku na mpaka sasa mimi mwenyewe nimeshapokea ruzuku
ya dola 5000 kwaajili ya kuniinua katika masuala yangu ya uchimbaji"alisema Negela
Hakuna maoni
Chapisha Maoni