HABARI ILIYOSHANGAZA JIJI-SERIKALI YAWARUKA WAANDISHI WA HABARI WALIOPIGWA NA POLISI,YASEMA HAINA TAARIFA HIZO,ISANGO AKIMBILIA MAHAKAMANI,SOMA HAPA KUJUA ZAIDI
MWANDISHI WA GAZETI LA TANZANIA DAIMA JOSEPHAT ISANGO AKIPIGWA NA POLISI |
Na Karoli Vinsent
HUKU wadau
mbalimbali wa Habari wakiwa wanalaani Vikali kitendo cha Jeshi la polisi
kuwapiga wanahabari wakati wakiwa kazini,tukio hilo lilitokea Mwishoni mwa wiki
iliyopita Makao makuu ya Jeshi la polisi nchini ambapo mwenyekiti wa chama cha
Demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman Mbowe alipofikishwa polisi,
Katika hali ya kushangaza Serikali imesema haina taarifa juu ya kupigwa kwa mwandishi,bali imesema inafahamu tu wanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema ndio waliokwenda makao makuu ya Jeshi la Polisi,na hawafamu kwamba kunawanahabari waliopigwa,
PICHANI NI MKURUGENZI WA IDARA YA HABARI MALEZO ASSAH MWAMBENE |
Kauli hiyo ya Kushangaza imetolewa leo jijini
Dar Es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya
Habari Maelezo,Asah Mwambene wakati alipokuwa anatembelea Mradi wa Maendeleo wa
Shirika la tanesco uliopo Mbagara Jijini Dar Es Salaam,licha ya kuzungumia
masuala mbalimbali kuhusu Tanesco kufikisha Miaka 50 ya kutuo huduma,
Ndipo Mwandishi wa Habari wa Gazeti
la Mwananchi alipomuuliza Mkurugenzi huyo kwamba yeye kiongozi wa Waandishi wa
habari anazungumziaje kitendo cha Jeshi la Polisi kuwapiga waandishi wa habari
walipokuwa kazini wiki iliyopita.
Ambapo Mwambeni ambaye vilevile pia ni Msemaji wa Serikali alisema
hana taarifa za kupigwa waandishi wa habari bali anacho fahamu yeye ni wanachama
wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema walikwenda polisi.
“Serikali haina taarifa za kupigwa kwa
waandishi Serikali inachojua ni wanachama wa chama cha Chadema ndio walikwenda
kwenye jeshi la polisi na sio waandishi wa habari,na tunachojua sio waandishi
wa habari waliopigwa,nakuomba tuzungumeze vitu vingine ”Alijibu Mwambene.
PICHANI NI MWANDISHI WA TANZANIA DAIMA JOSEPHAT ISANGO |
Baada ya Mwambene kuzungumza kauli
hiyo,alitoka pembene akawa anaongea na Mwandishi wa Gazeti la Habari leo ambaye
naye ni Miongoni mwa Waandishi wa Habari waliopigwa na jeshi la polisi katika
Tukio hilo huku akirekodiwa na mwandishi wa Mtando huu bila ya yeye kujua
kwamba mwandishi wa Mtandao huu anayafuatilia mazungumo hayo alisikika akisema
“Ni
mwandishi mmoja tu anayelalimia sana
kwenye Vyombo vya Habari,ni Yule Josephat isango wa gazeti la Tanzania daima Yule
tunajua kabisa ni mwanachama wa chadema kabisa maana aliwai kugombania Ubunge
kupitia chama hicho na tunachojua sisi na hata polisi waliokuwa wakimpiga
wanamjua Yule ni chadema ndio maana wakampiga unategemea serikali tufanyaje “alihoji
Mwambene.
Kauli hiyo ya Mwambene inatafsiriwa
tofauti na wadau wa Masuala ya Habari kwani kuzungumza huku kunazidisha maswali
mengi kutokana na Idara ya habari maelezo ndio inayowasimamia Waandishi pamoja
na Magazeti.
Kwa
Upande wake Mwandishi ambaye anashutumiwa na Mwambene Josephati Isango wa
Gazeti la Tanzania Daima,wakati alipokuwa anafanyiwa mahojianao maalum na
Mwandishi wa Mtandao huu jana jijini dare s Salaam,ambapo alisema kwa sasa
anajipanga kwenda mahakamani kumburuza mahakamani Cp Chagonja,Polisi watatu
waliompiga pamoja na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
“Nasahivi
nawasiliana na Wanasheria wangu watatu jinsi ya kwenda mahakamani kuwashitaki
polisi watatu,Cp Chagonja,waziri mkuu mizengo Pinda ambaye ametoa kauli ya
pigwa tu Bungeni nafanya hivi kupata haki ya kwetu sisi waandishi Habari”alisema
Isango
Hakuna maoni
Chapisha Maoni