KUMEKUCHA-CUF NAO WAUNGANA NA CHADEMA KUFANYA MAANDAMANO NA MGOMO NCHI NZIMA,LIPUMBA ALIVAA JESHI LA POLISI,SOMA HAPA KUJUA ZAIDI
PICHANI NI MWENYEKITI WA CHAMA CHA WANANCHI CUF PROFESA IBRAHIM LIPUMBA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI LEO JIJINI DAR ES SALAAM PICHA NA HABARI24.BLOGS |
karoli
Vinsent na Exaud Mtei wa Habari24.blogs
Chama
cha wananchi CUF leo kimetangaza kuunga mkono harakati zinazofanywa na chama
cha democrasia na maendeleo CHADEMA za kuandaa maandamano nchi nzima kupinga
kuendelea kwa bunge maalum la katiba na kusema kuwa chadema kipo sawa na
maandamano hayo ni halali na watatoa ushirikani wote katika maandamano hayo.
Akizungumzaa jumapili hii na wanahabari
jijini Dar es salaam mwenyekiti wa chama hicho profesa IBRAHIMU LIPUMBA amesema
kuwa CHADEMA kama chama cha siasa ni jukumu na ni haki yao kufanya maandamano
pale ambapo wataona kuna ubadhilifu wa fedha za wananchi unatokea katika nchi.
Aidha LIPUMBA akizungumzia sakata la
kuitwa na kuhojiwa kwa mwenyekiti wa CHADEMA na kiongozi wa kambi ya upinzani
bungeni mh FREMAN MBOWE amesema kuwa hakuna sababu yoyote ya msingi ya kumhoji
kjiongozi huyo kwani maandamano yote yanayoitishwa na CHADEMA yanafwata
taratibu zote ila kinachotokea ni polisi kutokujua sheria za maandamano.
Na kusema kumwita mh MBOWE ni kumdhalilisha
kiongozi huyo mkubwa wa upinzania wakati anatekeleza haki yake ya kikatiba.
“kazi ya polisi sio kuruhusu maandamano ya chama chochote,sisi tunatoa taarifa
tu kwa polisi ili watulinde,
na hatuombi kibali cha polisi kiufanya
kibali,polisi wanadhani kuwa sisi tunaomba kibali cha maandamano wakati ni haki
ya kikatiba kabisa ya kuandamana na kufanya mikutano ya adhara. Mh LIPUMBA
amesema kuwa CHADEMA sio chama cha kwanza kutangaza maandamano ya nchi nzima
kuhusu jambo la katiba kwani mapema baada ya hotiuba ya Rais KIKWETE aliyoitoa
wakati anafungua bunge la katiba chama cha mapinduzi nao walitangaza mikutano
na maandamano nchi nzima ambayo hayakupingwa na polisi ila anashangaa upinzani
kunyimwa haki hiyo ya msingi.
Katika hatua nyingine chama hicho cha CUF
kimelaani vikali kitendo cha kupigwa na kudhalilishwa kwa wanahabari nje ya
makao makuu ya polisi wakati wakifwatilia sakata la kuitwa mh MBOWE mwishoni
mwa wiki jana
Hakuna maoni
Chapisha Maoni