ZIMAMOTO MKOA WA ILALA WAOPOA MIILI MIWILI
Na Mussa Augustine
Jesh la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Ilala jijini Dar es Salaam, limeopoa miili miwili iliyokua inaelea kwenye Maji katika eneo la Stakishari Ukonga na daraja la Sarenda na kuikabidhi kwenye vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama kwa uchunguzi.
Kamanda wa Jeshi hilo Mkoa wa Ilala ,SACF Mabusi Peter, akizungumza leo na Waandishi wa Habari katika viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Zimamoto Duniani,amefafanua kwamba katika eneo la Stakishari mwili wa mwanamke anayekadiliwa kuwa na umri zaidi ya miaka 60 jana jioni uliopolewa kwenye Maji.
Pia mwili mwingine wa mwanaume anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka kati ya 21 hadi 26 umeopolewa leo majira ya saa tano asubuhi katika daraja la Salenda.
"Leo asubuhi tukiwa katika viwanja hivi vya Mnazi Mmoja tulipokea taarifa ya wito kuwa kuna mwili wa mwanaume asiyefahamika umeonekana ukielea katika daraja la Salenda na tukaenda kuuopoa pia jana tuliopoa mwili wa mwanamke maeneo ya Stakishari,miili hiyo tumeikabidhi kwenye vyombo vingine vya ulinzi na usalama kwa ajili ya uchunguzi," amesema.
Kamanda Mabusi, amesisitiza kuwa katika kipindi hiki cha mvua wananchi wanatakiwa kuwa na tahadhari wakati wa kuvuka mito ili kuepuka kusombwa na maji yanayoweza kusababisha vifo.

No comments
Post a Comment