BREAKING NEWS--CHADEMA YATANGAZA RASMI MAANDAMANO NA MGOMO NCHI NZIMA,YALIPOTEZEA JESHI LA POLISI,WASEMA LIWALO NA LIWE SOMA HAPA KUJUA ZAIDI
PICHANI KATIKATI NI Mkurugenzi wa Mafunzo na oganizasheni wa Chama cha chadema,Benson Sengo Kagaira wakati wa Mkutano na Waandishi Habari picha na Maktaba |
Na Karoli
Vinsent
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo Chadema
Kimetangaza rasmi kuanza maandamano pamoja na Migomo nchi nzima kwaanzia kesho
mpaka Jumamosi kushinikiza Bunge la Katiba lisitishwe kwa madai Bunge hilo limekuwa
likitekezea pesa za Watanzania huku
Katiba haipatikani.
Maandamano hayo yametangazwa mda huu
jijini Dar Es Salaam na Mkurugenzi wa Mafunzo na oganizasheni wa Chama cha hicho,Benson Sengo
Kagaira wakati wa Mkutano na Waandishi Habari ambapo alisema licha ya Jeshi la
Polisi kuwanyima Kibali cha kufanya Maandamano pamoja na Migomo ambayo ni haki
ya kikatiba kwa kila mtanzania,basi chama hicho kitaanza maandamano rasmi
kwaania kesho Jumatatu mpaka Jumamosi.
“Jeshi la Polisi nchini limetunyima
haki ya kufanya Maandamo ambayo kimsingi
ni haki ya kila Mtanzani kudai haki yake ambayo katiba imetamka wazi,basi
Kwaanzia kesho mpaka Jumamosi Tunatangaza Maandamano nchi nzima kupinga wizi
huu unafanyika Bungeni Dodoma na hatutamuogopa mtu yeyote,tena nawataka
watanzania wajitokeze kila walipo wajumuike katika kufanya Maandamo nchi nzima”alisema
Kagaira
Kagaira
alizidi kusema Maandamano haya yatafanyika nchi nzima na kila mkoa maandamano
hayo yataanzia kwenye ofisi za Chadema kwenye Mikoa hadi kwenye Ofisi za Mkuu
wa mkoa,
“Maandamano haya yatafanyika kwa kwa
awamu katika wiki zima,kwa upande wa Mkoa wa Dar Es Salaam tutafanya Jumatano
wiki hii na tutaelekea Ofisi za Waziri Mkuu na kwa upande wa Dodoma wataelekea Ofisi za
Bunge na mikoa mingine watachagua lini hasa katika wiki hii wataanza maandamamo
ila nimetoa maagizo kwa Viongozi wa Chadema wa Mikoa kuhakikisha wanachagua
siku yeyote ndani ya wiki hii kuanza maandamano,tena wasiogope polisi wala nani
kwasababu Polisi wamekuwa upande wa Chama cha Mapinduzi na Kuacha kazi yao kikatiba”alizidi
kusema Kagaira,
Vilevile Kagaira aliwataka
watanzania popote walipo kujiweka tayari kwa maandamano kwani maandamano hayo
ni ya amani na kusema Chadema haitoweza kukubali kuyumbishwa na Jeshi la polisi
ambalo limekuwa likifanya mambo kibabaishaji
Kwa
Upande wake Wakili wa Chama hicho John Mallya alisema wamejipanga kisheria
katika kuhakikisha haki ya msingi ya maandamano inapatikana na kuwataka
wanachama pamoja na wapenzi wa chama hicho kujitokeza kwa wingi kwenye maandamo
hayo’
“Tumeomba kibali cha maandamano Jeshi
la polisi linatukatalia na kusema Bunge la katiba liko kisheria kama ndio hivyo
mbona bunge lenyewe likiuka sheria ya mabadiliko ya katiba kwa kitendo chake
cha kujigeuza na kuanza kuchukua maoni kutoka kwa wananchi ambayo sio kazi yake,kwahiyo
nawaomba watanzania wote kujitokeza kwa wingi kwenye maandamano”alisema Mallya.
Katika hatua nyingine chama hicho
kimelaani vikali kitendo cha Jeshi la polisi kupiga waandishi habari wiki
iliyopita wakati wa walipokuwa wakichukua taarifa juu ya mwenyekiti wa Chadema
Freeman Mbowe.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni