GAZETI LA TANZANIA DAIMA LAZIDI KUPATA NA MAJANGA,MSAJILI WA MAGAZETI AZIDI KULIANDAMA,WENYEWE WAKUBALI YAISHE SOMA HAPA KUJUA
PICHANI NI MHARIRI WA GAZETI LA TANZANIA DAIMA EDSON KAMUKARA,PICHA NA MAKTABA |
Na Mhariri wa Gazeti hilo
KATIKA
machapisho ya gazeti hili, toleo namba 3554 la Agosti 27, 2014 na toleo namba
3555 la Agosti 28, 2014 tulikuwa na habari zenye vichwa: Kikwete anywea na
Kikwete ‘alamba matapishi’ yake.
Vichwa hivyo vya
habari vilileta mkanganyiko mkubwa serikalini, na Ofisi ya Msajili wa Magazeti,
kupitia Idara ya Habari (MAELEZO) ilitutaka tutoe maelezo, kwa msingi kuwa
vichwa hivyo vya habari vilikuwa vinamdhalilisha Rais.
Tulifafanua
maana halisi ya vichwa hivyo na habari zilizoandikwa lakini ufafanuzi wetu
haukumridhisha , msajili na kutaka tuombe radhi tena.
Tumeona ni
jambo la busara zaidi kuomba radhi kwa mara nyingine tena kwakuwa hatukukusudia
kumdhalilisha Rais
Kwa kuzingatia
misingi ya kitaaluma na hasa baada ya kubaini mkanganyiko uliosababishwa na
ukali wa maneno ya vichwa hivyo vya habari, tumeona ni jambo la kiungwana
kuomba radhi kwa mara ya pili katika ukurasa wa mbele habari husika
zilipoandikwa.
Na kwa kuwa
tumegundua kwamba aliyekwazwa ni Rais mwenyewe, tumesukumwa na utu na taaluma
kumwomba radhi Rais mwenyewe kupitia gazeti hili.
Habari iliyokuwa
na kichwa cha habari: Kikwete anywea, haikulenga kumdhalilisha au kumshusha
hadhi Rais, bali kuelezea kwamba baada ya mvutano wa muda mrefu kuhusu umuhimu
wa yeye kukutana na viongozi wa Umoja wa katiba ya Wananchi (UKAWA), hatimaye
amelegeza msimamo, amekubali kukutana nao.
Ushahidi ni
kwamba vikao hivyo vimekuwa vinaendelea kwa nyakati tofauti. Ukweli ni kwamba
visingefanyika kama rais na washauri wake wasingelegeza msimamo.
Kuhusu
habari iliyosema: Kikwete ‘alamba matapishi yake’, lengo lilikuwa kusisitiza
jinsi Rais Kikwete alivyobadili msimamo ghafla na kutetea jambo alilowahi
kupinga kwa nguvu zote.
Hii ilitokea
baada ya Rais Kikwete kusema hadharani kwamba serikali yake inafikiria kutoa
elimu bure, sera ambayo katika uchaguzi wa mwaka 2010 ilikuwa ya Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), huku yeye na chama chake wakiibeza.
Tunachukua
fursa hii kumuomba radhi Rais pamoja na watu wote walioguswa kwa namna moja au
nyingine na vichwa vya habari vya magazeti husika
Hakuna maoni
Chapisha Maoni