HABARI NZITO LEO--LOWASSA AIPASUA IDARA YA USALAMA WA TAIFA,AWATUMIA HADI WAKINA MBOWE NA MBATIA KUINGIA IKULU,SOMA HAPA ZAIDI
PICHANI NI WAZIRI MKUU ALIYEJIUZULU EDWARD LOWASSA PICHA NA MAKTABA |
Na Karoli Vinsent
MBUNGE wa Monduli mkoani Arusha, Edward Ngoyai Lowassameanza mikakati
kabambe ya kushika madaraka ya nchi, mara baada ya Rais Jakaya Kikwete kumaliza
muda wake mwakani.
Taarifa za uhakika ambazo mtandao huu, imezipata zinasema kwamba mikakati hiyo ni pamoja na kumteua Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Usalama wa Taifa (TISS-DG), Colnel Apson Mwang’onda kuwa Mwenyekiti wa mtandao wa kumwingiza Lowassa Ikulu.
Taarifa zinasema kwamba ndani ya mtandao huo wamo wajumbe kutoka kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Freeman Aikaeli Mbowe (Mwenyekiti wa Chadema-taifa) na James Francis Mbatia (Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi).
Katika hali ya kustaajabisha, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ametengwa kwa sababu si mzaliwa wa kaskazini kama ilivyo kwa Mbowe na Mbatia ambao hata siku moja hawajawahi kumshambulia Lowassa kisiasa.
Taarifa za uhakika ambazo mtandao huu, imezipata zinasema kwamba mikakati hiyo ni pamoja na kumteua Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Usalama wa Taifa (TISS-DG), Colnel Apson Mwang’onda kuwa Mwenyekiti wa mtandao wa kumwingiza Lowassa Ikulu.
Taarifa zinasema kwamba ndani ya mtandao huo wamo wajumbe kutoka kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Freeman Aikaeli Mbowe (Mwenyekiti wa Chadema-taifa) na James Francis Mbatia (Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi).
Katika hali ya kustaajabisha, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ametengwa kwa sababu si mzaliwa wa kaskazini kama ilivyo kwa Mbowe na Mbatia ambao hata siku moja hawajawahi kumshambulia Lowassa kisiasa.
“Hawa wajumbe wa Ukawa, kila mmoja ana malengo yake. Hawa akina Mbatia na Mbowe ni kwa sababu ya ukaskazini. Wanampigania mkaskazini mwenzao, ndio maana huoni hata siku moja wakimshambulia Lowassa,” anasema mtoa habari.
“Lipumba yeye anaipigania Zanzibar kwa kuwa ikichukua dola, atafaidika nayo. Anaona kuwa Zanzibar ikiwa nchi na kuwa na madaraka yake, itakuwa rahisi kwake kufanya mabadiliko Tanzania Bara,” anasema.
Wajumbe wengine ambao mdau wa Monduli ameona mikakati ya Lowassa ni kuwaingiza kwenye mtandao huo vigogo waliomwingiza Rais Kikwete madarakani.
Wajumbe hao ni Mbunge wa zamani wa Lindi Mjini, Mohammed Abdulaziz na Mbunge wa sasa wa Lushoto mkoani Tanga, Beatrice Shelukindo. Pia yumo Pindi Chana-Naibu waziri wa Jinsia na Watoto.
Taarifa za uhakika zinasema Jumamosi ya tarehe 16 Agosti 2014, majira ya saa tano asubuhi, Mbatia alikwenda nyumbani kwa Apson ambako walijichimbia ndani kwa mazungumzo yaliyochukua saa 4. Mazungumo hayo yaliisha majira ya saa nane mchana.
Baada ya kuondoka kwa Mbatia, aliingia Abdulaziz ambaye alifanya mazungumzo na Apson mpaka majira ya jioni.
Taarifa zinasema kwamba Abdulaziz ambaye ni ndugu wa Mbunge wa zamani wa Mchinga, Mudhihir Mudhihir amejiunga na mtandao kufanya kazi kama aliyofanya mwaka 2005 wakati wa kumwingiza Rais Kikwete madarakani.
“Abdulazizi amekasirika sana kutengwa na Rais Kikwete. Kwani anaona kuwa hajatendewa haki kwani alifanya kazi ya ziada kama mwanamtandao mwandamizi, lakini alibahatika tu kuwa mkuu wa mkoa wa Tanga na kisha Iringa, halafu basi,” anasema mtoa habari.
Hata hivyo, haikuweza kufahamika mara moja walichozungumza wadau hao na Apson, lakini kuna habari kuwa Mbatia alipewa maelekezo mapya kuhusu nguvu ya Ukawa.
“Ndiyo maana unaona kuwa Mbatia ameibuka, kusemea kauli Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema kueleza kuwa hakuna mwenye mamlaka kisheria kuvunja au kusitiza Bunge la Katiba, akielezea kuwa ni ya kinafiki na kwamba upo uwezekano wa kuahirisha vikao kwa muda mpaka mwafaka wa kitaifa utakapopatikana.
Mbatia akasema kuahirisha Bunge kunawezekana kama ambavyo iliwezekana kusitishwa vikao vya Bunge hilo Aprili mwaka huu kupisha Bunge la Bajeti na kubadilishwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kinyemela kwa kuongeza idadi ya siku za Bunge la Katiba kutoka 70 hadi 90 mpaka kuwa muda wowote ambao utaonekana unafaa.
Akizungumza na waandishi waHabari jijini Dar es Salaam, Mbatia alisema kauli iliyotolewa na Jaji Frederick Werema imejaa unafiki.
Katika mkutano huo ambao Mbatia pia alieleza maazimio ya mkutano wa halmashauri kuu ya chama hicho uliofanyika Agosti 14, mwaka huu, alihoji kama Bunge la Katiba haliwezi kusitishwa, iliwezekana vipi kulisitisha kupisha Bunge la Bajeti.
Mbatia alisema ni jambo la ajabu kuona watu wakitunga sheria kwa ajili ya kukinufaisha kikundi cha watu wachache na akasisitiza kuwa kufanya hivyo ni sawa na kuwahadaa Watanzania.
“Kama katika awamu ya kwanza tuliweza kuliahirisha Bunge la Katiba kupisha Bunge la Bajeti bila kuwapo kwa sheria, pia tunaweza kulihairisha katika awamu ya pili ya Bunge hilo kupisha maridhiano. Mshikamao wa kitaifa ni zaidi ya Bunge la Bajeti na kitu chochote,” alisema.
“Tatizo la Watanzania ni kuwa na umaskini wa fikra uliobebwa na ujinga, fitna, umbeya, kusema uongo, kujenga chuki katika jamii na uvivu wa kufikiri. Maridhiano ya kitaifa ni njia pekee ya kunusuru mchakato wa Katiba.”
Alisema wajumbe wanaoendelea na vikao vya Bunge hilo mjini Dodoma wanakusudia kupitisha rasimu kwa ajili ya kukibeba chama kimoja cha siasa na siyo kwa ajili ya masilahi wa Watanzania.
“ Dola inaundwa kwa msingi wa maridhiano, siasa inafuata baadaye. Hilo lilifanyika Zanzibar na nchi nyingi barani Afrika zilizokumbwa na machafuko ya wenyewe kwa wenyewe wakati wa kuandika Katiba,” alisisitiza.
Akizungumzia maazimio ya halmashauri kuu, Mbatia alisema: “Tumeitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuliweka hadharani Daftari la Kudumu la Wapigakura lililoboreshwa mwaka 2010, kutokana na hivi karibuni tume hiyo kueleza kuwa hakuna daftari. Tunajiuliza kama halipo hata walioshinda chaguzi zilizopita siyo halali.”
Alisema kwa kauli hiyo maana yake ni kwamba ukifanyika uchaguzi wowote nchini hakuna atakayeweza kupiga kura, kutaka mfumo wa uandikishaji wapigakura wa kieletroniki (BVR) uwekwe wazi na kusimamiwa na Tume Huru ya Uchaguzi yenye weledi, kutokana na kukiri hadharani kuwa iliyopo sasa imeshindwa kazi.
“Tunaitaka Serikali itamke wazi tarehe ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na usimamiwe na Tume Huru ya Uchaguzi kwa kutumia Daftari la Kudumu la Wapigakura lililoboreshwa,” alisisitiza
Source MwanahalisiForum
Hakuna maoni
Chapisha Maoni