TCU YACHARUKA YAKIFUNGIA CHUO KIKUU CHA IMTU,SOMA HAPA KUJUA ZAIDI
Na Karoli
Vinsent
TUME ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) Imekifungia kwa
mda,Chuo kikuu cha tiba na Sayansi IMTU kutofanya udahili kwa Wanafunzi wapya wa Mwaka
wa Masomo 2014-2015,kutokana na chuo hicho kukiuka sheria ya inayosimamia Vyuo
Vikuu nchini.
Uamuzi huo wa kikifungia Chuo hicho
Umetangazwa mda huu Jijini Dar Es Salaam na Kaimu Mtendaji wa Tume ya Vyuo
Vikuu nchini (TCU) Profesa Magishi N
Mgasa wakati wa Mkutano na Waandishi wa habari ambapo alisema maamuzi hayo yamefikiwa
baada kikao cha Dharura kilichoitishwa na (TCU) wiki iliyopita na kujadili
taarifa ya timu iliyotathimini chuo hicho,
Ambapo kikao hicho kikabaini mapungufu
makubwa katika chuo cha IMTU yakiwemo matatizo ya uongozi,kukosa wahadhiri
wakutosha na wenye sifa,kutokuwepo na Vifaa pamoja na kudahili wanafunzi bila
hata kuwa na taratibu zilizowekwa na tume,
Profesa
Mgasa alisema kwa kufanya hivyo chuo cha IMTU imekiuka sheria ya namba 5(1),sura
ya 346 ya sheria za Tanzania ambayo inakitaka chuo Kikuu chochote kufuata
taratibu zilizowekwa na tume,
Vilevile Profesa Mgasa alizidi kusema
baada ya Tume kubaini makosa hayo,ndipo wamefikia maamuzi ya kukifungia chuo
cha IMTU kufanya udahili kwa wanafunzi wapya wa Mwaka 2014-2015,mpaka pale
itakakaporekebisha mapungufu yaliyotajwa na Tcu,
Pia tume imetoa notsi ya miezi 3 kwa chuo cha
IMTU,kuanzia tarehe 16 mwezi huu kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza na endapo
chuo hicho kikikaidi basi TCU haitosita kuwachukulia hatua kali ikewemo hata
kukifungia kabisa.
Aidha Profesa Mgasa aliwataka
wanafunzi nchini wasijiunge na chuo Kikuu chochote bila ya kufuata maelekezo kutoka Tume ya vyuo
Vikuu nchini (TCU).
Hakuna maoni
Chapisha Maoni