LOWASSA NA RICHMOND,SITTA NA BUNGE LA KATIBA,SOMA HAPA ZAIDI
Septemba 15 mwaka huu,
saa 2:00 usiku wakati akiahirisha kikao cha Bunge, Mwenyekiti wa Bunge la
Katiba Samwel Sitta alisema fedha zitakazookolewa katika uendeshaji wa Bunge
hilo hazitarudishwa Serikalini bali zitatafutiwa kile alichokiita‘utaratibu’.
Nikimnukuu Sitta, alisema “Sababu tutakuwa tumeokoa fedha kiasi fulani sasa zile zisiwe za kurudi huko huko tena. Lazima tufanye utaratibu kwamba zitumike katika kazi iliyokusudiwa”.
Nikimnukuu Sitta, alisema “Sababu tutakuwa tumeokoa fedha kiasi fulani sasa zile zisiwe za kurudi huko huko tena. Lazima tufanye utaratibu kwamba zitumike katika kazi iliyokusudiwa”.
“Nadhani mtanielewa vizuri wakati huo na tutakuwa tunalirudia hili tangazo ili kulielewa vizuri,” alisema Sitta huku ukumbi wa Bunge ukilipuka kwa furaha za wajumbe wa Bunge hilo.
Sitta alienda mbali na kusema kama wajumbe watamaliza vizuri na kutoka na Katiba inayopendekezwa kwa ajili ya kupigiwa kura, Itakuwa ni zawadi nzuri sana kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Hakuna tafsiri nyingine yoyote ambayo unaweza kuitumia kutafsiri kauli hii ya Sitta zaidi ya kusema kuna mipango ya kugawana, ama kuzitafutia matumizi mbadala, fedha zitakazookolewa.
Hii ni kauli mbaya sana na ya dharau kwa Watanzania masikini wanaojiminya usiku kucha kuhakikisha kuwa wanalipa kodi. Ni kauli ya dharau kubwa kwa wafanyakazi wa nchi hii wanaokamuliwa kwa kulipa kodi ya mishahara (Paye).
Nilitarajia Sitta angesema fedha zitakazookolewa zitapelekwa kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu wanaohitaji mikopo au zikapelekwa kwenye ujenzi wa maabara katika shule zetu za Kata.
Ningemwelewa Sitta ambaye anaamini Watanzania watamuona anafaa kuwa Rais 2015, kama angesema pesa hizo zielekezwe kwenye miradi ya maji, umeme vijijini, zahanati na miundombinu ya barabara.
Sitta anatoa kauli kama hii akijua wazi kuwa Serikali ambayo yeye ni sehemu yake, haina pesa kiasi ambayo bajeti ya 2013/2014 ilikuwa na upungufu wa Sh 1.8 trilioni katika bajeti yake ya maendeleo.
Kwa maneno mengine, miradi mingi ya maendeleo iliyokuwa imepangwa kutekelezwa mwaka wa fedha wa 2013/2014 haikutekelezwa kabisa kutokana na upungufu wa fedha.
Leo hii anapokosa uzalendo wa kuwahurumia Watanzania hawa maskini na kulazimisha eti fedha zitakazookolewa zisirudishwe Serikalini bali zitatafutiwa ‘utaratibu’ mwingine, inatia kichefuchefu.
Kazi iliyokusudiwa ilikuwa ni kuandika Katiba inayopendekezwa, sasa kama mmefikia mwisho na kufanikiwa kuokoa kiasi cha fedha, kazi nyingine ambayo ilikusudiwa anayoisema Sitta ni ipi? Kwa wajumbe 130 waliosusia Bunge hilo wakiwamo wajumbe wa umoja wa Katiba ya wananchi (Ukawa), ni dhahiri karibu kiasi cha Sh2.3 bilioni zitaokolewa, ndizo anazozilenga Sitta?.
Namshukuru na kumpongeza sana Katibu wa Bunge hilo, Yahya Khamis Hamad ambaye alionyesha naye kushangazwa na kauli hiyo ya Sitta na kusema hawapewi fedha za kubaki.
Nikimnukuu Hamad anasema “Mimi hayo niliyasikia lakini kwangu pia ni ya ajabu kwa sababu siye fedha tuliyonayo haitoshi sasa hiyo ya kubaki mimi sijui. Sijui labda yeye anajua sitaki kumsemea”.
Sitta anafahamu pia kuwa Katiba hii anayojivuna nayo kuwa itakuwa bora katika ukanda wa Afrika, itahitaji utashi wa kisiasa wa Rais ajaye, habanwi kikatiba kuanzia pale watakapoishia.
Kwa maneno mengine, kama Rais ajaye ataamua hataki kuanza na Katiba iliyowagawa Watanzania, ni dhahiri mamilioni ya shilingi za Watanzania maskini zitakuwa zimepotea.
Sitta alichotakiwa kukifanya ni kuhakikisha anafanya juu chini ili Bunge hilo liokoe kiasi kikubwa cha pesa kadri iwezekanavyo na kukirudisha Serikalini
Hakuna maoni
Chapisha Maoni