Zinazobamba

DOKTA REGINADI MENGI AZIDI KUONYESHA UTU WAKE KWA WATANZANIA,SOMA ZAIDI HAPA

PICHANI NI Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya Ipp media Dr Reginadi Mengi

   Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya Ipp media Dr Reginadi Mengi ameahidi kuanzisha tunzo ya wachimbaji wadogo wa madini ili kuwawezeshesha  wanawake wajimbaji wa madini wadogowadogo Tanzia (TAWOMA) kujikwamua kiuchumi.

Akizungunza leo Jijini Dar Es Salaam  wakati wa  hitimisho la  warsha ya Wanawake wajimba madini wadowadogo Tanzania Mengi alisema kuwa ili  kuwawezesha wanawake kuamka ni lazima wanawake wenyewe kuelewa kwamba wanaweza maana hakuna aliyezaliwa kuwa daraja la pili.
  “Ni lazima wanawake waseme kwamba wanaweza wenywewe na wakishajitambua hivyo watembee katika hali ya kuweza na sio kusema tunaweza na badala yake wakatembea katika hali ya kuonekana wamekwisha kushidwa”alisema

“ Hakuna aliyezaliwa kuwa wa daraja la pili kila mtu amezaliwa wa kwanza na hivyo ni lazima jitihanda zifanyike ili kuendelea kubaki kuwa wa kwanza na hatimaye kuwa mshindi,wanawake nataka niwambie kwamba mnaweza na mkijiamini kuwa nyini ni wa pekee basi mtafika katika kile manachokikusudia”aliongeza


Dr Mengi ameongeza kuwa atashughulikia swala la changamoto ya soko la madini  inayowakabili wachi
mbaji wadogo hao kuendelea kuzalisha  huku wakiwa na mategemeo ya kufika mbali kimafanikio siku za usoni.
               “Niwaahidi kushugulikia maboresho ya soko la ndani kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuwawezesha nyinyi kuendelea kuwa na moyo wa kufanya kazi hizi maana katika sheria ya nchi ya mwaka 2004 kunakipengere kinachomtaka mtu yeyote mwenye uweo kumsaidia mtanzania na mimi nimekuwa nikifanya hivi kwa sababu hata mimi nianzia chini,”alisema.
                  Washa iliyofanyika  kwa siku mbili  iliwahusisha wanawake wajichamba madini, ambamo mwanzoni mwa ufunguzi warsha hiyo mwenyekiti wa chama cha wanawake wajimba madini ( TAWOMA ),Yunisi Nyegere  alisema changamoto zinazo kikumba chama hicho mojawapo ni kukosekana kwa soko la ndani,uhaba wa vitendea kazi,na wanachama kutokuwa na elimu dhidi ya  madini.
Mwisho…

Hakuna maoni