NI MUNGU TU NDIO ATAKAYEYAOKOA MAGAZETI YA NIPASHE,TANZANIA DAIMA NA MAWIO,SASA SERIKALI YAWAEKEA MTEGO MDOGO MDA WOWOTE KUFUNGIWA,SOMA HAPA KUJUA ZAIDI
Na karoli
Vinsent
SERIKALI ya
Rais Jakaya Kikwete imezidi kuuzika uhuru wa Habari nchini kutokana na sasa
kuanza kuvifungia vyombo vya Habari hususani Magazeti,baada ya hivi sasa
serikali yake kujiweka tayari kuyafungia magazeti ya Nipashe,Tanzania Daima
pamoja Mawio,Mtandao huu unaripoti
Taarifa za kuaminika ambazo mtandao huu
umezipata zinasema serikali imejipanga kuyafungia magazeti hayo kutokana na
habari wanazoziandika ambazo serikali inaziita ni za uchochezi,
Kwa mujibu wa Vyanzo mbalimbali zinasema
serikali imekasilishwa na Habari wanazoziandika magazeti hayo kuhusu mwenendo
wa Bunge Maalum la Katiba ambazo wanadai
habari hizo zinaleta mgongano kwa wananchi,
Mpashaji huyo wa Habari aliuambia mtandao huu
kwamba kwasasa serikali imejipanga kuhakisha inayafungia magazeti hayo.
“Sikiliza sahivi serikali imechoka sana
na mwenendo wa haya magazeti nchini,yaani yamekuwa yakiaandika habari ambazo
ukizisoma utazijua tu ni za uchochezi tu,na tayari msajili wa magazeti
ameshaawaandia barua wahariri wamegazeti hayo lakini bado wanakuwa wabishi
wanaendelea kuandika habari tofauti kuhusu bunge la Katiba”alisema Mpashaji
huyo wa habari kutoka wizara ya habari.
Chanzo hicho kilizidi kusema Gazeti la
kila siku la Nipashe limeonywa sana ili wahariri wake wamekuwa wakimkaidi
msajili wa Magazetii,baada ya kuandikwa Barua ya kuonywa na Msajili wa Magazeti
lakini bado wamekuwa wakibisha.
Mwandishi wa Mtandao huu alishuhudia Barua
aliyoandiwa Mhariri wa Gazeti la Napashe kutoka Msajili wa Magazeti Raphael
Hokororo yenye kumbukumbu namba 77/319/01/80 ambapo barua hiyo ilikuwa na
kichwa cha Habari Habari uliyochapisha
inayohusu Bunge la Katiba,katika barua hiyo msajili alitoa malalamiko yake
kwenye gazeti hilo tarehe 15 Sepmtemba
2014 toleo namba 0578237 uliochapisha Habari iliyosemeka “BUNGE LA KATIBA
HASARA”
Habari hiyo ilizidi kusema Mabilioni
yake yangetosha kujenga Zahanati 600,na Noti zake zikipangwa barabarani ni Dar
mpaka Bukoba,ambapo Msajili wa Magazeti
nchini amemtaka Mhariri wa Gazeti hilo kwenda kutoa maelezo kwa madai bunge
hilo lipo kisheria.
Kwa upande wake Gazeti la Mawio nalo
liko katika njia panda kutokana na wakati wowote nalo litafungiwa kutokana na
Gazeti hilo kutofahamika wamiliki wake haswa,
Kwa mujibu wa Mpashaji wetu aliyoka
ndani ofisi ya Mkurugenzi wa Habari Maelezo ambaye akutaka jina lake kutajwa
kwenye Mtandao huu alisema Serikali hususani ofisi ya Msajili wa magazeti
imefanyiwa rafu sana katika uanzishaji wa Gazeti la Mawio.
“Nahilo gazeti la Mawio sikufichi lina
mda mfupi sana na lazima litafungiwa mda wowote,kwasababu serikali imeshajua
hilo gazeti wamiliki wake ni walewale waliokuwa wanamiliki gazeti liliofungiwa
na serikali kwa mda usiojulika la mwanahalisi ambao ni Saed Kubenea na Mtu
mmoja wa fedha kutoka ndani Chadema,kwa mfumo huu gazeti la Mawio wamiliki wake
pamoja na Mhariri wake wa sasa wanaotambulika na ofisi ya msajili wa Magazeti
sio wale”
“ Ambacho wakina kubenea walichokifanya ni
kuwafwata wamiliki wa Gazeti la Mawio anbao walishindwa kuliongoza Gazeti hilo
mpaka likafilisika, wakina kubenea wakaenda kule wakawapa Fedha wamiliki
hao,wakaachiwa gazeti,sasa ingebidi wale waje kuleta taarifa kwa msajili wa
Magazeti lakini wao hawakwenda,matokeo yake sasa gazeti likifanya makosa
wamiliki wake wanaenda wakina kubenea na msajili anawakataa anasema hawa sio
wamiliki wanaotambulika kwa msajili na ndio maana serikali inajipanga
kulifungia Gazeti hili ”alisema Mpashaji huyo wa Habari
Kwa upande wa Gazeti la Tanzania Daima
nalo lipo wakati wowote kufungiwa kutokana na kile anachokiita msajili wa
Magazeti nchini ni kuwa linaandika habari za upotoshaji,
Gazeti hilo linashutumiwa kutokana na
Vichwa vya Habari wanavyoviandika ambavyo ofisi hiyo ya Msajili inaviona ni vya
kichochezi ni toleo namba 3554 la Agosti 27, 2014 na toleo namba 3555 la
Agosti 28, 2014 tulikuwa na habari zenye vichwa: Kikwete anywea na Kikwete
‘alamba matapishi’ yake, na Rais Kikwete Anywea
Ndipo msajili
wa Magazeti nchi alitaka gazeti la Tanzania daima kuomba Radhi kwa uzito ule
ule wa Mwanzo na gazeti hilo likafikia uamuzi huo na kuomba Radhi kwenye
machapisho yake,Licha gazeti hilo kuomba Radhi lakini bado gazeti hilo
linawindwa na mda wowote litafungiwa na serikali kutokana habari zake ambazo
zinagusa maslai ya Serikali.
Kupewa Vitisho
hivi kwa wamiliki wa Magazeti nchini,pamoja na Wahariri,kunaendana na sawa na
kauli aliyosema Waziri Kivuli wa Wizara ya Habari Joseph Mbilinyi “SUGU” wakati
anawasilisha Makadilio ya bajeti ya Wizara hiyo ya Habari bungeni ya Kambi ya Upinzani,alisema
“Kwa sasa zipo fikra
miongoni mwa wadau wa vyombo vya habari kwamba uhuru wa habari nchini unazidi
‘kuwambwa msalabani’ kwa sababu ya utatu wa hatari ambao umetengenezwa na
Serikali ya CCM, kwenye Wizara ya Habari, Vijana, Michezo na Utamaduni. Utatu
huu hatari unaundwa na waziri mwenyewe Dk. Fenela Mkangara ambaye mbali ya
kwamba si mwanahabari, si mwanasanaa, si mwanamziki wala si mwanamichezo,
taarifa zinaonesha kuwa amekuwa na dhamira ya kupambana na vyombo vya habari,
ambao ni wadau wake, tangu alipoteuliwa.”
Hotuba hiyo ilimnukuu mmoja wa waandishi waandamizi nchini, ambaye aliandika haya kuhusu huyo Waziri;
“Waziri mwenye dhamana Dk. Fenella Mukangara kwa muda mrefu amekuwa na nia ovu dhidi ya vyombo vya habari. Julai mwaka jana (akimaanisha 2012) tukiwa Hoteli ya Dodoma mjini Dodoma, wakati tunafanya mazungumzo rasmi na Waziri Mukangara, walikuwepo Theophil Makunga, Pili Mutambalike, Neville Meena na marehemu Alfred Mbogola na wengine, Dk. Mukangara alitoa kauli iliyotushtua wengi na sasa ndipo tunaona inatekelezeka kwa vitendo.”
Mwandishi huyo aliongeza kwa kunukuu maneno ya Waziri Mukangara ambaye amenukuliwa akisema;
“Nikipata fursa Mwananchi nitalifuta, mimi linanikera sana. Tena na Nipashe nao naona wanakuja, ikibidi nitawafungia tu, mimi siogopi kitu.” Hayo ni maneno ya Waziri anayetakiwa kuwa mlezi wa vyombo vya habari!
Mwandishi huyo katika makala yake akaendelea kuandika hivi;
“Baada ya kauli hii tuliendelea na mazungumzo mengine, lakini Meena akatuambia kuwa Dk. Mukangara aliwahi kutoa kauli kama hii ofisini kwake walipokwenda akina Jesse Kwayu, Meena na Absalom Kibanda kuomba Gazeti la Mwanahalisi lifunguliwe. Mwanahalisi alilifungia kwa muda usiojulikana…”.
Hizi ni tuhuma nzito sana kuweza kukaliwa kimya na Serikali yoyote makini. Ni jambo la ajabu kuwa pamoja na uzito wake, si tu kwamba hazikupata majawabu yanayostahili, bali hazikujibiwa kabisa. Anayebeba tuhuma hizo hadi leo anakaa meza ‘moja’ na Rais wakati wa vikao vya Baraza la Mawaziri.
Katika kukamilisha hoja ile ya utatu wa hatari, hotuba ile ya Kambi ya Upinzani, ikaendelea kusema;
“Si Waziri Mukangara mwenyewe wala mtu mwingine yeyote kwa niaba yake, amewahi kukanusha maneno hayo aliyonukuliwa akiyasema hadharani mbele ya wadau ambao yeye anapaswa kuwa kiongozi na mlezi wao. Kutokana na mwenendo wa Waziri Mukangara wa kupambana na vyombo vya habari, unaofumbiwa macho na mamlaka iliyomteua, labda kwa bahati mbaya au sehemu ya mkakati wa serikali hii ya CCM. Uhusiano wa waziri na vyombo vya habari ulifikia hatua mbaya zaidi, baada ya wadau wa habari waliokutana Oktoba 9 mwaka jana, kufikia maazimio kadhaa, ikiwemo lile linalosema;
“Kusitisha kuandika, kutangaza na kupiga picha shughuli zozote zitakazowahusisha au kuratibiwa na Mheshimiwa Fenella Mukangara na Assah Mwambene hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo. Adhabu hiyo inaanza mara moja kuanzia leo.”
Hotuba ikaongeza;
“Hapo juu kwenye moja ya maazimio ya wadau wa habari, ametajwa Assah Mwambene, huyu ni Mkurugenzi wa Habari Maelezo. Mkurugenzi huyu ambaye amewahi kufanya kazi kwenye vyombo vya habari kama mwandishi, pamoja na kwamba kwa majukumu yake hayo alipaswa kuwa mtu wa karibu kama mwelekezi na kiongozi kwa wadau wake (au wenzake), kwa kushirikiana na Waziri Fenella Mukangara, amekuwa ni mwiba kwa utendaji wa vyombo hivi, akihusika kuuweka uhuru wa habari na uhariri katika sintofahamu kubwa.
“Kitendo cha Mkurugenzi wa Habari Maelezo kufanya maamuzi makubwa ya kuyatisha magazeti ya Mwananchi na Rai, kutimiza wajibu wa kuendelea kuhabarisha, kwanza bila kuwa na msingi wowote wa kisheria na pili bila kuwasiliana na wakubwa wake wala wasaidizi wake, kama ilivyotamkwa na aliyekuwa Naibu Waziri Amos Makala, ni jambo ambalo linathibitisha jinsi alivyo sehemu ya utatu huu tunaozungumza hapa

Hakuna maoni
Chapisha Maoni