Zinazobamba

TAMKO ZITTO KUHUSU RASMU YA KATIBA KUTOKA KWA WANANCHI HILI HAPA

 

Wanaharakati wakisoma tamko lao hii leo, mambo makubwa ambayo wamesisitiza kwa wajumbe wa bunge maalum ya katiba wanapaswa kufanya ni kuhakikisha kuwa madaraka ya wananchi yanarejeshwa ili aweze kumuwajibisha kiongozi wake, pili umiliki wa ardhi kwa wawekezaji ni lazima kuwe na ukomo pamoja na suala la maji lazima lipewe kipaumbele


 

liundi akifafanua jambo mbeel ya waandishi wa habari mapema hii leo


Muda mfupi baada ya Endrew Chenge kutangaza rasmu ya katiba inayo pendekezwa, wanaharakati ngazi ya jamii wameibuka na kusema kuwa rasimu hiyo inakasoro nyingi ambazo zinahitaji kufanyanyiwa marekebisho na kama hatua za marekesho hatachukuliwa basi katiba hiyo itakuwa na uhai mdogo ikilinganishwa na katiba ya mwaka 1977,
Akizungumza na mtandao huu mapema hii leo, Mkurugenzi wa Mtandao wa TGNP Bi Liliana Liundi ameweka wazi kuwa rasmu hiyo imejaa vitu vya kung'ata na kupuliza hatua ambayo amesema kama hatakuwa wagumu awa kufanya marekebisho rasmu itakuwa nzuri sana,


Liundi ameongeza kusema kuwa, Rasmu hiyo kwa kiasi kiubwa imewabana wananchi katika kuakikisha inamuajibisha kiongozi yeyote ambaye hajtimiliza majukumu yake"

Unajua Rasimu ya katiba imeipa uwezo bunge la jamhuri ya muungano kumuwajibisha Rais pindi akishindwa kutekeleza majukumu yake na akienda kinyume na sheria na taratibu za nchi. Lakini rasimu hii imewanyima wananchi  haki yao ya msingi ya kumuwajibisha kiongozi (Mbunge/diwani) waliemchagua kwa kura zao halali pindi anaposhindwa kutekeleza majukumu na ahadi alizozitoa wakati wa kampeni kwa wananchi. sasa hii si haki Alisema Liundi.
Naye  mwezeshaji wa mdahalo wa wanaharakati hao Bw. Badi Idarusi Ameuambia mtandao wa fullhabari ya kwamba kilichofanywa na wajumbe wa bunge la katiba ni kizuri lakini kuna mambo ambao tunadhani yanahitaji kupewa kipaumbele katika rasmu hii, 
alitaja mambo hayo kuwa ni pamoja na suala la maji ambalo ni lazima liwe kipaumbele kwani kwa sasa watanzania wengi wameshindwa kupata maji safi na salama kwa wakati kutokana na haki hiyo kutopewa kipaumbele,
Sasa mama zetu wamekuwa wakitembea umbali mrefu kutafuta maji lakini rasmu hii haikuliona hilo hivyo tunadai suala hili lazima litafutiwe namna ya kuliingiza katika rasmu hii,
Aidha alipohojiwa kuhusu muda wa kuanza kudai hayo mambo ambayo kimsingi muda wa kukusanya maoni umeonekana tayari umekwisha, Darusi amaesema kuwa bado kuna muda takribani siku 8 ambazo kama tutazimia vizuri tunaweza kubadilisha hali ya hewa na tukawa na katiba ya wananchi.
Ndugu yangu mwandishi mambo yanawezekana kabisa mua bado tunao tunachoomba wenzetu wawe wasikivu ili maslahi ya mtanzania yawez kufikiwa, hii nchi ni ya kwetu sote, aliongeza Bwana Badi
aidha katika mambo mengine ambayo wanaharakati hao wanayadai kwa nguvu zao zote ni pamoja na
Kutokana na hayo tulio yaeleza hapo juu tunadai yafuatayo;

i.                           Tunadai katiba itamke uwiano wa 50/50 katika nafasi na ngazi zote za maamuzi kati ya wanawake na wanaume kuanzia ngazi za chini kabisa hadi taifa.

ii.                        Tunadai haki ya kupata maji safi na salama iwe ni haki ya kikatiba ili kuweza kuwapunguzia wanawake mzigo wa kutembea umbali mrefu wa kutafuta maji.

iii.                       Tunadai rasimu hii ya katiba ibadilishe sifa ya kiwango cha elimu ya mbunge kuwa kidato cha nne.

iv.                       Tunadai mawaziri wasiwe miongoni mwa wabunge ili kuimarisha utendaji na uwajibikaji wa mihimili yote mitatu kwa kila mhimili kujitegemea.

v.                        Tunadai katiba iweke ukomo wa vipindi kwa wabunge kukaa madakani na iweke mfumo mzuri wa kuwawajibisha viongozi wasiotimiza majukumu yao kwa wananchi.

vi.                       Tunadai rasimu iweke mfumo mzuri wa kuwasaidia makundi ya walio pembezoni kuweza kupata huduma bora za afya bila ya kikwazo.

vii.                     Tunadai kipengele cha ukomo kwa wawekezaji kutumia ardhi ili kuweza kuepusha migongano na migogoro ya ardhi kati ya wananchi na wawekezaji katika suala zima la umiliki wa ardhi.

viii.               Tunadai katiba iunde chombo maaalum kitakachosimamia haki za wanawake katika maeneo yote ya kijamii, kisiasa, na kiuchumi

ix.                      Tunadai rasimu ya katiba itambue haki ya kupata elimu kutoka elimu ya awali hadi elimu ya juu ili kuweza kuondoa matabaka katika jamii na sio kuweka utaratibu tu wa upatikanaji wa elimu.

x.                         Tunadai rasimu hii ya katiba ifute kipengele cha Benki kuu ya Tanzania (BOT) kutowajibishwa na kudhibitiwa na  mtu au mamlaka yoyote ya kiutendaji ili kuimarisha mfumo wa uwajibikaji.

Tamko hili limesainiwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao kwa niaba ya washiriki wa semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS) na wanaharakati  wa ngazi ya jamii leo tarehe 27/9/2014.

Hakuna maoni