KAMANDA TIBAIGANA AMSHANGAA IGP MANGU,NI KUHUSU MAANDAMANO YA UPINZANI SOMA HAPA
Katika mahojiano maalumu na gazeti hili
nyumbani kwake Buganguzi wilayani Muleba, Kamishna Tibaigana alisema suala la
maandamano halikumsumbua kwa kuwa alielewa kuwa sheria inayaruhusu, hivyo
alichokuwa akifanya ni kuwaita viongozi wa vyama vinavyotaka kuandamana na
kufanya nao makubaliano ya namna maandamano hayo yanavyopaswa yafanywe kabla ya
kuyaruhusu.
“Pengine hiyo ndiyo sababu sikuwahi kushambuliwa kwa maneno ya kejeli au
matusi na wanasiasa kwa kuwa sikuwahi kuzuia maandamano yao bila sababu na hata
kama kulikuwa na sababu niliwaita na kuwaeleza na tulikubaliana.
“Kikubwa ni kujenga tabia ya kuwaita viongozi wa waandamanaji na
kujadiliana nao, vinginevyo wanaweza pia hata kukufikisha mahakamani wakipinga
kuzuiwa maandamano yao,” alisema Tibaigana ambaye alikumbana na sakata la kudai
maandamano wakati akiwa Kamanda kwenye mikoa ya Tanga, Arusha na Dar es Salaam.
“Nilikuwa nawaita viongozi nakaa nao tunakubaliana. Hata kama
ningeambiwa na kiongozi gani nisitoe kibali, kama hakuna sababu za kweli,
nilikataa kwa kuwa kisheria mimi ndiye nawajibika kama vyama vikishtaki. Ili
uzuie maandamano unapaswa kuwa na sababu za msingi ambazo ukiwaeleza
waandamanaji wanakuelewa.”
Tibaigana anakumbuka jinsi CUF kilivyoandaa maandamano makubwa
kushinikiza kuundwa kwa serikali ya mseto visiwani Zanzibar baada ya
kutoridhishwa na matokeo ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2005, lakini anasema kutokana
na msimamo wake, haikuwa vigumu kwake kuruhusu jambo hilo.
“Wakati wa uongozi wangu CUF ilikuwa na nguvu sana, lakini mimi sikuwa
na tatizo nao. Walipotaka kibali cha kuandamana niliwapa bila woga na tuliishi
vizuri,” anaeleza Tibaigana.
Vuguvugu la maandamano pia lilitanda wakati wa maandalizi ya ziara ya
Rais wa zamani wa Marekani, George Bush nchini kutokana na wasomi na baadhi ya
wanaharakati kutaka kufanya maandamano kupinga vitendo vya taifa hilo kubwa
dhidi ya raia wa Palestina na sehemu nyingine ambako wananchi wasio na hatia
walikuwa wakiuawa.
“Nilichofanya ni kukutana nao na kuwaeleza njia ambazo wangeweza kutumia
katika maandamano hayo na hali ilikuwa shwari,” alisema Kamanda Tibaigana.
Katika kipindi chake cha uongozi wa Polisi Dar es Salaam, Kamanda
Tibaigana pia alikumbana na vurugu za kidini ambazo zilisababisha askari mmoja
kupoteza maisha, lakini anasema kwa kushirikiana na wadau wengine, walijipanga
na hali ikawa shwari.
Alivyomng’ang’ania
Ditopile
Moja ya matukio makubwa wakati akiwa Kamanda wa Kanda ya Dar es Salaam
ni tukio la mkuu wa zamani wa Mkoa wa Tabora, Ditopile kumuua dereva wa
daladala baada ya kutokea kutoelewana barabarani, hali iliyolazimu sheria
kufuata mkondo wake. Jeshi la Polisi lilitakiwa limkamate mkuu huyo na
kumfikisha mahakamani.
Ditopile alituhumiwa kufanya mauaji hayo Novemba 5, 2006. Akidaiwa
kumuua kwa kumpiga risasi dereva wa daladala, Hassan Mbonde. Alikamatwa na
kufikishwa mahakamani, lakini alifariki dunia Aprili 20, 2008 wakati kesi yake
ikiendelea.
Kamishna
Tibaigana anasema tukio hilo lilimtia katika msukosuko mkubwa kutokana na
kupata shinikizo kutoka kwa viongozi mbalimbali waliokuwa wakitaka asitekeleze
wajibu wake wa kumkamata na kumfikisha mahakamani.
“Nilihojiwa na baadhi ya viongozi
baada ya kuamuru Ditopile akamatwe, lakini nikasisitiza kuwa amevunja sheria
kama walivyo wahalifu
Hakuna maoni
Chapisha Maoni