VITA DHIDI YA MISHAHARA HEWA YAIBUA MENGI, jumla ya Billioni 50 zimepona, waliohusika sasa kukiona cha moto
WAZIRI AKIFAFANUA |
Habari zilizotufikia hivi punde ni kwa kwamba ile vita ya kati ya wizara ya fedha na watumishi hewa sasa imefikia patamu ambapo baadhi ya taasisi kubwa nchini zimekutwa zikinufaika na watumishi hewa ambao hata taarifa zao hazijulikani,
Akizungumza na mtandao huu mapema hii leo, baada ya kurudi kutoka Zambaia alikoenda kushiriki mkutano wa kufanya nchi hizo mbili kuwa na kituo kimoja cha ushuru wa forodha, naibu waziri wa uchumi na fedha Mh. Mwigulu Nchemba amesema vita hiyo kwa sasa imeanza kuonyesha matuda yake baada ya kufanikiwa kuponya jumla ya shilingi bilioni 50 kwa mwezi mmoja uliopita,
Waziri Nchemba amesema mpaka sasa toka waanze mfumo mpya wa kulipa pesa kupitia akaunti za waajiriwa wenyewe wamebaini kuwepo kwa watumishi hewa hususani katika mashirika ya umma ambayo yamekuwa yakipokea fedha kwa umoja wake na kuanza kuzigawa kwa watumishi wao
Nchemba amesema mfumo mpya wa ulipaji wa fedha umebaini pia jumla ya wafanyakai hewa 14,000 kwa njaia ya benki na wafanyakazi 1,900 ambao walikuwa wanachukua pesa kupitia madirishani wameonekana kuwa hewa,
Akifafanua hatua ambazo serikali yake itachukua dhidi ya watendaji ambao walikuwa wakinuafaika na mishara hewa kwa muda mrefu, Waizri Nchemba amesema tayari suala hilo limeshafikishwa katika ofisi ya takukuru na jeshi la polisi ili wachukuliwe hatua kama wezi wengine
"Hawa ni kama wezi wengine hivyo hatua ambayo tumechukuwa ni kulifikisha suala hilokatika vyombo vinavyohusika ili hatua ambazo zinastahili ziweze kuchukuliwa|" aliongeza waziri Nchemba
Aidha akizungumzai kuhusu suala la uwazi katika mgawanyo wa fedha kutoka hazina kwenda halmashauri mbalimbali, Nchemba amesema kuna baadhi ya sintofahamu miongoni mwa halmashauri wakizani kuwa kuna baadhi ya wenzao wanapata fedha nyingi kuliko wenzao, sasa wameamua kuweka kila kitu hadharani ili ifahamike ni kiasi gani kimepangwa kwa ajiri ya halmashauri zao,
Tutaweka Taarifa zote katika mtandao ili taarifa hizo ziweze kupatikana kwa wakati na wahusiaka.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni