Zinazobamba

pato la taifa Tanzania kwa mwezi ni hili hapa, WAZIRI AAPA KUFIKISHA TIRIONI

Mwigulu nchemba akifaanua jambo mbele ya waandishi wa habari. Picha na maktaba
 Naibu waziri wa fedha ameaapa kuongeza pato la taifa kwa mwezi na kusema kwamba sasa timu yake iko msituni kusaka na kuzipa manya yote ambayo imekuwa ikipelekea kupotea kwa fedha nyigi kutoka katika vyanzo mbalimbali
Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu mapema hivi karibuni, waziri Mwigulu nchemba amesema kumekuwa na mianya mbalimbali ambayo watu wamekuwa wakitumia katika kukwepa kulipa kodi ili kukuza pato la taifa ambalo ndio msaada mkubwa wa kukuza uchumi wa nchi

Nchemba amesema kwa sasa taifa linakusanya jumla ya shilingi bilioni 800 kwa mwezi pato ambalo limekuwa kutoka bilioni 500 kwa mwezi katika kipindi cha mwaka 2010
Akifafanua sababu za kukua kwa pato hilo la taifa kwa kasi ya namna hiyo kwa kipindi kifupi, Nchemba amesema hiyo ni kutokana na ukweli kuwa mianya mbalimbali imekuwa ikizibwa na hivyo kuongeza pato hilo kwa kiasi kikubwa
Tumezipa mianya mingi sana ya ukwepatiji wa kodi ambapo sasa fedha zinaonekana kuingia katika mfuko wa serikali, aidha katika hatua nyingine, mwigulu amekiri baadhi ya fedha kuendelea kuingia katika mifuko ya watu wasio wema na kwamba ameamua kuanza kuifuatilia hali hiyo ili kuondoa mianya yote ya ukwepaji wa kodi
Kuna kodi nyingi wananchi wanalipa lakini kodi hizo zimekuwa zikingia katika mifuko ya watu wachache , kodi kama ya taka, maduka a majengo ni kodi muhimu lakini imekuwa hakusanyi kwa usahihi hali inayopelekea kuendelea kupoteza mabilioni ya shilingi,

Hakuna maoni