kuna nini zaidi kama mgomo wa mbowe utaruhusiwa
Asubuhi na mapema chombo kimoja cha habari kiliripoti ya kwamba ule mgomo ambao ulitakiwa kushika hatu yake mapema hii leo, uliingia dosari baada ya kinara wa mgomo huyo kuitwa makao makuu kujielezwa ni kwa nini anataka kuitisha mgomo huo usio na kikomo?
Katika kuitikia wito huo mkuu huyo wa kambi ya upinzania anadaiwa kwenda katika mkutano huo na jeshi la polisi ili akiambana na mawakili wake wa chama Akiwamo wakili maarufu hapa nchini Wakili Mabele marando, Tundu Lissu na Kibatara ambaye alipata umaarufu mkubwa kupitia kesi ya Zitto Kabwe,
mpaka sasa mambo bado hayajulikani kama mgomo huo utakuwepo ama ndiyo umeyeyuka, Si nia yangu hapa kuelezea umuhimu mgomo lakini najaribu kujiuliza mwenyewe hivi kunanini hasa kama mgomo huo utaachiwa uende hewani,
Ni Kwa maslahi ya nani hasa tunaamua kuingia barabarani ama kuzuia mgomo huo, Mgomo huo unafaida gani hasa na hasara zake ni zipi? na kwani hasa mgomo huo uwe sasa, haya yote ni maswali ambayo hakika majibu yake ni vurugu mtupu
Wanaharakati mbalimbali ambao wamehojiwa na mtandao huu mapema hii leo kuhusu kadhia hiyo ambayo imegusa vichwa vya habari vingi hapa nchini, wamesema mjadala huo unaonekana kuipa maslahi baadhi ya kundi fulani ambalo linauchu na madaraka,
naweza kushawishika na hilo, lakini je tuko tayari kuondoa amani yetu kwa maslahi ya kundi fulani, tuko tayari kuhatarisha maisha yetu kwa faida ya nani hasa????
Jana niliwasikiliza kwa makini umoja wa wanafunzi makini wa chuo kikuu, wakilaani kauli ya Mh. Freemani Mbowe wakisema kauli ya kiongozi huyo ni ya Kichochezi na Iliyolenga kuchafua amani iliyopo, hakika sikupuuza maono hayo ya vijana muhimu katika taifa hili,
labda niwaachie swali wadau wangu hapa, hivi ni kweli tunahaja ya kuanza na mgomo wa mbowe kwa sasa
Hakuna maoni
Chapisha Maoni