DIKTETA SITTA AZIDI KUPINGWA KILA KONA NA BUNGE LAKE,NAO HAKI ZA BINADAMU WAZIDI KUCHACHAMAA,SOMA HAPO ZAIDI
Mkurugenzi wa
uwezeshaji na uwajibikaji wa kituo hicho IMELDA URIO wakati akisoma tamko la
kituo hicho kuhusu mwenendo wa mchakato wa katiba,
|
Karoli Vinsent na Exaudi Mtei wa
Habari24.blogs\
HUKU Ikiwa bado wadau mbalimbali nchini wakiendelea
kupiga kelele kutaka bunge maalum la katiba lisimamishwe mara moja kwa kile
wanachodai ni wizi wa fedha za watanzania ndani ya bunge hilo,
Nao Kituo cha sheria na haki za Binadamu
nchini LHRC wameibuka na kumtaka na Rais wa jamhuru ya muungano wa Tanzania
kuchukua hatua mara moja ya kulisimamisha bunge hilo hadi maridhiano ya ukweli
yatakapopatikana.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es
salaam na mkurugenzi wa uwezeshaji na uwajibikaji wa kituo hicho bi IMELDA URIO
wakati akisoma tamko la kituo hicho kuhusu mwenendo wa mchakato wa katiba hadi
hapa ulipofikia,
Ambapo amesema kuwa wamekuwa
wakifwatilia kwa ukaribu mchakato huo na kutoa maoni yao ambayo kwa kiasi
kikubwa yamekuwayakipingwa kwa maslahi ya kisiasa.
BI EMELDA anasema kuwa kumekuwa na
kauli za kuwachanganya watanzania juu ya uwezo wa Rais kulivunja bunge hilo
akitolea mfano kauli ya mwanasheria mkuu wa serikali aliyoitoa mnamo tarehe 17
mwezi wa nane kuwa Rais hana mamlaka ya kulivunja bunge hilo kwa madai ya
kutokuwepo kwa kipengele cha sheria ambapo amesema kuwa kauli hiyo haina maslahi
wala uchungu wa watanzania ambao ndio walipa kodi zinazowalipa kodi wajumbe
hao.
Aidha ametolea mfano kauli nyingine
aliyoitoa mwenyekiti wa bunge hilo mh SAMWELI SITTA ambapo alisikika akisema
kuwa pamoja na makubaliano ya kuahirisha bunge hilo hadi baada ya uchaguzi na
kusema upigaji kura wa kifungu kwa kifungu uko pale pale pamoja na uwezekeno wa
theluth mbili kutopatikana, huku akitaka kuwashirikisha watanzania walioko nje
ya nchi,wagonjwa na wale walioko hijja,
Kituo cha sheria wamesema kuwa mwenyekiti huyo
anafanya hayo yote huku akijua wazi kuwa anapotosha umma. Katika hatua nyingine
LHRC wamesema kuwa swala la uchaguzi halihusiani kabisa na mchakato wa katiba
mchakato wa katiba unaweza kabisa kuendelea na uchaguzi sambamba kwani rasimu
ya katiba hususani ibara ya 268 inatoa kipindi cha mpito cha miaka minne kabla
ya kuanza kutumia katiba mpya.
Hivyo kusitisha mchakato wa katiba kwa
kisingizio cha uchaguzi ni kosa kubwa sana ambalo linatokana na kuwaachia
wanasiasa mchakato huo ambapo wamesema kuwa wanasiasa kazi yao kubwa ni
kuangalia maslahi yaoya kuwepo madarakani na si maslahi ya wananchi. LHRC ni
wadau wengine waliojitokeza kupinga mwenendo wa bunge hilo huku kukiwa na wimbi
la watu mbalimbali wakiwemo wanasiasa,asasi za kiraia ambao nao wamekuwa
wakitaka bunge hilo liahirishwe mara moja
Karoli Vinsent na Exaudi Mtei wa
Habari24.blogs

Hakuna maoni
Chapisha Maoni