KUMEKUCHA--DK SLAA AWACHANACHANA CHEYO NA DUVUTWA,AFICHUA SIRI NZITO KUTOKA KWAO, NAYE MNYIKA ATEMA CHECHE KWA JESHI LA POLISI,SOMA HAPA KUJUA
PICHANI NI VIONGOZI WA CHADEMA WAKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI LEO |
Na Karoli
Vinsent
HALI ya
Kisiasa nchi yaonekana kutokuwa nzuri baada ya wanasiasa kuanza kugeukana
kutokana na taamaa ya fedha baada ya SIRI za mazungumzo ya Mkutano kati ya Rais
Jakaya Kikwete pamoja na Viongozi wa Vyama vya kisiasa vilivyo chini ya Kituo
cha Demokrasia (TCD),sasa siri za Kikao hicho zaanza kuvuja.
Mkutano huo ndio ulitoa maazimio ya
kulisitisha bunge la katiba na kuifanyia marekebisho katiba iliyopo ya mwaka
1977 kwa madai bunge la katiba la sasa aliwezi kutengeneza Katiba,
Naye, Katibu Mkuu wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Dk Wilbroad Slaa ameibuka na kufichua siri za Mkutano huo na kusema Mwenyekiti wa Kitoa cha Demokrasia (TCD) John
Cheyo pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha UPDP Mhe Fahmi Dovutwa walikuwa wakimuomba Rais jakaya Kikwete
asilisitishe Bunge la katiba kwa madai watakosa posho katika Bunge hilo,
Siri hizo zimefichuliwa leo Jijini
Dar Es Salaam na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Dk Wilbroad
Slaa wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari,ambapo Dk Slaa alisema
anasikitishwa na siasa za hovyo walizokuwa nazo John Cheyo na Fahmi Dovutwa kwani wanasiasa hao ni wapenda
posho.
“Mimi nawashangaa watu wanaopoteza mda
kuwasikiliza wanasiasa wahovyo kama hao kwasababu wakati wa mkutano na
Rais Kikwete na TCD, Katibu Mkuu wa CCM , Abdulrahman Kinana
aliandaa Tamko lilosainiwa na Prosesa Lipumba,James Mbatia,pamoja na mimi
mwenyewe kwenda kwa Rais Kikwete tena Tamko hilo likuwa likimtaka Rais Kikwete
alisitishe bunge la katiba kwa madai bunge hilo aliwezi kutengeneza katiba”
“Na Rais Kikwete alikubaliana na
sisi kwamba bunge maalum la katiba haliwezi kutengeza katiba,hawa wakina
Dovutwa,cheyo na Mrema wakasema kwamba Rais ukilisitisha bunge la katiba mwezi
huu tutakosa posho,na Rais huyo alivyokuwa ni muoga akubaliana nao na kukubali
bunge litafune pesa mpaka tarehe 4 octoba”alisema Slaa,
Dokta Slaa alizidi kusema Umoja wa katiba
UKAWA hauwezi kubishana na Wanasiasa hao kwakuwa vyama hivyo ni miradi ya chama
tawala cha CCM.
“Hivi
leo chama cha CUF,NCCR-mageuzi-Chadema tupoteze mda wetu kubishana na vyama
vilivyosajiliwa zaidi ya Miaka kumi na tano kwa msajili wa vyama vya kisiasa
lakini mpaka leo hakina hata mwenyekiti wa serikali za mtaa wala mbunge
kitatuambia nini,harafu mwenyekiti wao wanaibuka kwenye bunge hilo la katiba na
kusema Upinzani hupo Bungeni,huu si uozo mtupu”alizidi kusema Slaa,
Vilevile
Dokta Slaa hakusita kumzungumzia Mwenyekiti wa TLP Mhe Augustine Lyatonga Mrema
na kusema mwenyekiti huyo wakati wa kikao hicho cha TCD na Rais Kikwete kila
alipokuwa akipewa nafasi na Rais Kikwete alikuwa akiishia kusema Rais Jakaya
Kikwete amzuie James Mbatia asikwenda kugombania kwenye Jimbo lake la Vunjo
badala ya kuzungumzia masuala ya katiba,ndipo ikamfanya Rais Kikwete awambie
wajumbe wakikao hicho kwamba wachukulia hari hiyo ni ya Utani kwa kitu
anachosema,
Katika Hatua nyingine chama
hicho Kikuu cha upinzania nchini kimesema Maandano na Migomo iliyotangazwa na
Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe juu ya kushinikiza Bunge la katiba
lisitishwe kwa madai bunge hilo linapoteza pesa za wanannchi bure, iko pale
pale na wala chama hicho akiogopi kauli zenye lengo ya kuwatisha tama
zinazotolewa na Jeshi la polisi.
Hayo aliyesema Mwanasheria
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Tundu lissu,ambapo alisema hoja
wanazosema jeshi la polisi kwamba Maandamo pamoja na Migomo nchi nzima hazina
ukweli kwani maandamo ni haki za Msingi kikatiba,
Vilevile Tundu Lissu ambaye ni Mbunge wa
Singida Mashariki CHADEMA alisema chama hicho kimesikitishwa na ufanyi kazi wa
hovyo wa Jeshi la polisi nchini,kutokana na Jeshi hilo kumwandikia barua
Mwenyikiti wa chama hicho Freeman Mbowe kwenda kwenye mahojiano huku
kikishindwa kuweka kosa wanalomuitia,
“Jamani wanahabari huu ndio upuuzi
wa jeshi letu la polisi ambalo lipo Kikatiba lakini ni la hovyo kutokana na kutojua sheria,maana Jana tarehe 17 tulipata
barua kutoka Jeshi la Polisi likimtaka Mwenyekiti wetu aende polisi makao makuu
kwa mahojianao cha kushangaza barua yenyewe haina hata kosa la wanalomwitia”
“Tukashaurina jana kwenye
kamati kuu tukakubaliana aende tu kwenye hayo mahojiano,maana tunajua,Hawa wahuni
wasije wakatuletea matatizo”alisema Gwiji huyo wa Sheria kutoka Chadema.
Naye Naibu Katibu Mkuu bara John
Mnyika alisema wakati Mwenyekiti wa Chama hicho anavyokwenda Polisi kuitikia
wito alioitiwa chama hicho kimejipanga kutoa wanasheria waliobobea kwenda
kumtetea mwenyekiti wa Chama hicho.
“Wakati ,wenyekiti wetu wa Chadema
atakapokuwa anakwenda kutoa maelezo Jeshi la polis hatasindikizwa na jopo la
wanasheria waliobabea maana chama chetu ndicho kinaongoza kuwa na wenye sheria
waliobobea na pia tunawataka wanasheria wate wanaoishi mkoa wa Dar es
Salaam,kujitokeza kwa wingi polisi makao makuu kwa lengo la kwenda kumtetea
mwenyekiti wetu”alisema Mnyika
Hakuna maoni
Chapisha Maoni