Zinazobamba

SIRI YA MBOWE KUCHAGULIWA TENA CHADEMA HII HAPA,NDIZO SABABU ZILIZOWAFANYA WANACHAMA KUMPOTEZEA ZITTO KABWE,SOMA HAPA KUJUA ZAIDI

Freeman Mbowe

Na karoli Vinsent
   HUKU Mkutano mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema ukiwa umalizika   tukishuhidia  uchaguzi  wa ndani wa Chama hicho ukimalizika huku kukiwa na ushindani kwenye ngazi mbalimbali ,
           Baada ya uchaguzi huo tumeshudia Kuchaguliwa tena katika nafasi ya mwenyekiti Freeman Mbowe ambaye amepita bila hata kupigwa kutokana na mshindani wake kujiondoa dakika za mwisho,
            Baada ya Mbowe kuchaguliwa katika nafasi hiyo ya Mwenyekiti tumeshuhidia akimrejesha tena katika Nafasi ya ukatibu Mkuu wa chama hicho Dk Wilbroad Slaa,huku akiweka sura mpya kwenye Nafasi ya Naibu katibu mkuu akimpa John Mnyika pamoja na Mwandishi wa habari Kijana kabisa Salum Mwalim kwenye Nafasi ya Naibu katibu mkuu Zanzibar,
          Leo katika Makala hii fupi nitazungumzia sababu ya wajumbe wa mkutano huo mkuu kuona umuhimu wa kumrejesha Mbowe na Dk Slaa katika nafasi zao,na sababu hizo ni kama ifuatavyo


          Mwaka, 2005 Freeman Mbowe alinadi ilani ya Chadema iliyobainisha kuwa Chadema itabadilisha mji wa Dodoma kuwa mji wa Vyuo vikuu. Baada ya Rais  kikwete kushinda akachukua fedha kwenye mifuko ya kijamii ya PSPF na NSSF na kuanzisha chap chap chuo kiuu cha UDOM. Matatizo ya kudandia hoja kwa kiongozi huyo ni kuwa mpaka leo CAG analalamika kuwa mifuko hiyo ina hali mbaya kifedha pesa za mifuko zilizokowa hazijarejeshwa.

        Mwaka, 2010 Dr Slaa alinadi ilani ya Chadema iliyosema Chadema itatoa elimu bure kuanzia kidato cha kwanza hadi sita.Hivi karibuni tumesikia Rais Kikwete akiwa mjini Morogoro ametangaza kuwa Serikali inaangalia uwezekano wa kuondoa ada mpaka kidato cha nne. Amesahau kuwa 2010 walimtukana Dr Slaa 2010 kuwa anapiga porojo zisizowezekana.kwa bahati mbaya sana imewachukua ccm miaka 4 kujua kuwa alichonadi Dr Slaa kinafaa.

        Mwaka 2005 freeman Mbowe aliasisi matumizi ya helikopta kwenye kampeni za kusaka urais. CCM ilitumia nguvu nyingi sana kushambulia matumizi ya helikopta kwa hoja dhaifu ya gharama. Mwaka 2010 chadema iliendelea kutumia helikopta na CCM wao wakatumia helikopta 2 na wakati mweingine 3. Iliwachukua ccm miaka 5 kugundua kuwa msururu wa magari 20 kwenye kampeni zao ni ghali kuliko helikopta mmoja ya Mbowe. CCM hawajawahi kumshukuru Mbowe na Ubunifu wake bali waliuchukua tu ubunifu huo kimya kimya na kwa aibu 2010.

            Mwaka 2010, Dr Slaa alinadi sera ya chadema ya kuwapa watanzania afya ya Bure - yaani matiabu yawe ya bure kama enzi za mwanzo za mwalimu Nyerere kwa watanzania wote. Sasa hivi serikali inasema
watoto chini miaka 5 na wazee matibabu yao ni bure. Hata hivyo, hospitalini hali haiko hivyo, kwa wazee na watoto. Matatizo ya kuiga ni kufanya jambo hilo hovyo hovyo.Hata hivyo, tunawashukuru kwa kutambua kuwa sera ya Chadema inatekelezeka na inawezekana.

          mwaka 2010 Dr Slaa alisema Chadema wakiingia madarakani gharama ya vifaa vya ujenzi kama sementi, mabati nk vitashuka kwa zaidi ya 50% ya gharama ya sasa (ya wakati huo 2010) kwa kuondoa kodi ili wananchi maskini waweze kujenga nyumba zao.
mpaka sasa serikali iko kimya kuhusu hili pengine hili litawachukua zaidi ya miaka 5 au zaidi ili kuielelewa. Nadhani tunahitaji kuwaombea Mungu awafanulie.

           Mwaka 2010 Dr Slaa alinadi ilani ya Chadema kuwa Chadema tukiingia madarakani tutaanzisha mchakato wa katiba mpya ndani ya miezi 3. Baada ya JK kuingia madarakani kiaina alidandia hoja hiyo na kuanzisha mchakato huo bila ridhaa ya ccm na bila kujali kuwa haukuwepo kwenye ilani ya ccm, matokeo yake tunayaona sasa.

          Mwaka 2010 Freeman Mbowe alimshirikisha Prof Lipumba na wakakubaliana kuibuka na UKAWA. Leo hii ushirikiano huu wa Chadema, CUF na NCCR (UKAWA) ambao Mbowe ni moja wa mwasisi mkuu ndo mjadala wa kitaifa kiasi kwamba wiki iliyopita Rais kikwete amewaita IKULU baada ya kugundua kuwa bila UKAWA hakuna KATIBA MPYA. Lazima tukubaliane kuwa bila ubunifu huu wa Mbowe leo hii katiba ingeandikwa na wangerejesha serikali mbili Kinyume na maoni ya wananchi yalikusanywa na tume ya Warioba bila kash kashi yo yote.

        Kwa hiyo, basi, sababu ya kwanza kuiendesha serikali kutoka nje na ndo maana sishawishiki kuwabadilisha viongozi                hawa wanaoiendesha serikali kutoka nje. Kwa maoni yangu, viongozi wote wawili Dr Slaa na Mbowe wabaki kwenye nafasi zao. Haya ni maoni yangu na ninaamini ndo msimamo wa wanachadema walio wengi. Hapa sijagusia mafanikio yao kwenye                 kuijenga Chadema mpaka ikasambaa nchi nzima kwenye ngazi ya mabalozi wa nyumba kumi /nyumba tano. Hiyo ni makala mengine na ni sababu ya pili ya kwa nini ninawapigia debe viongozi hawa wabakie kwenye nafasi zao.
Nawasilisha

Hakuna maoni