HABARI NZITO LEO-UFISADI WA IPTL,MBUNGE KAFULILA AIBUKA NA KUMKABA KOO CAG,AFICHUA RAFU INAYOTAKA KUFANYWA NA SERIKALI SOMA HAPA KUJUA ZAIDI
Na karoli
vinsent
SAKATA la Ufisadi Fedha Sh200 bilioni
zilizohifadhiwa kwenye akaunti ya Escrow zilitolewa na kulipwa kwa Kampuni ya
Pan African Power (PAP),ambazo zinadaiwa kuibwa na watendaji wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete,mapya yanazidi kuibuka.
Kutokana na Mbunge wa Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila amekuja juu
na kumtaka Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kutoa ripoti mara moja ya
uchunguzi aliyotumwa na Bunge ili umma ufahamu ukweli kuhusu sakata hilo,
Kauli ya Kafulila imekuja huku kukiwa
na Taarifa juu ya kustaafu kazi kwa Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali Ludovick
Utoh wiki hii kikatiba,mkaguzi huyo ambaye Bunge
lilimuagiza yeye CAG na Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza tuhuma hizo za uchotaji wa
fedha hizo.
Wasiwasi huo
umesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mbunge wa Kigoma Kusini (NNCR-Mageuzi)David
Kafulila wakati wa Mkutano na Waandishi
wa Habari,ambapo Kafulila alitoa masikitiko yake kwa Mkaguzi Mkuu wa Serikali
kushindwa kupeleka Taarifa Bungeni ya uchunguzi huo, badala yake ameipeleka
Serikalini harafu yeye mwenyewe akijua mda wake wakustaafu teyali umefika.
“Jamani
inasikitisha sana CAG anashindwa kupeleka taarifa za uchunguzi kwenye Bunge
ndio lilomtuma kisheria,sasa leo nimesikia taarifa ya ripoti nzima ameipeleka
serikalini ambapo sio kulikomtuma, Hata
hiyo (report) taarifa ya (Takukulu) ilipaswa kuwasilishwa kwa Bunge
kwani ni azimio la Bunge lilioagiza (Takukulu) kuchunguza baada ya Spika
kukataa hoja yangu ya kuunda kamati teule. Sasa PCCB amekabidhi Taarifa kwa
Rais Alhamisi kimyakimya.sasa kama si njama za kutoka kuuzima ukweli nini:”alihoji
Kafulila
Kafulila
alizidi kusema Kitendo cha Mkaguzi mkuu
wa Hesabu za Serikali CAG,kustaafu bila hata kupeleka taarifa ya uchunguzi wake
kwenye bunge kunazidisha mashaka juu ya
uchunguzi wenyewe,kwani ingebidi CAG apeleke taarifa zima ya uchunguzi wake na
ukweli.
“Ndugu zangu wanahabari hizi ni
fedha nyingi sana zaidi ya bilioni 200,ni fedha zingewekeza kwenye masula ya
maendeleo Taifa lingefika mbali lakini leo Fedha hizi zimeibwa watendaji
wachache,sasa kitendo cha CAG kustaafu bila hata kamati yake ijatoa taarifa ya
uchunguzi wake kunanipa mashaka sana na tunasikia mara taarifa imepelekwa
serikalini jamani mbona kuna utendaji mdogo hapa wa Viongozi wetu, ”Alizidi
kusema Kafulila.
Mbunge Kafulila ambaye anakesi mahakama kuu iliyofunguliwa na Kampuni
ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Pan Afrikan Power Solutions
Limited (PAP) na Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni hiyo, Harbinder Sigh Seth,
ambapo amefungua kesi hiyo kwa madai ya
Sh. bilioni 310 kwa Mbunge wa Kigoma
Kusini kwa kile anachokiita ni kuchafuliwa .
Alipoulizwa na Waandishi wa Habari kwamba
kuzidi yeye kuendelea kulizungumzia suala hilo haoni anaingilia upande wa
mahakama kutoka na kesi yenyewe kuwapo mahakamani,Kafulila alisema Kesi iliyopo
mahakamani hawezi kumzuia yeye kusema ukweli kwani pingamizi lilowekwa na
kampuni hiyo kwamba mahakama inamzuia Kafulila asingumzia suala hilo kwenye
vyombo vya Habari,bado mahakama haijatoa hukumu la pingamizi hilo.
Aidha Kafulila aliwataka wanasiasa,Watanzania
pamoja na Vyombo vya habari kutoufumbia macho Ufisadi huu wa pesa uliofanywa na
Watendaji wa Serikali ya Rais Kikwete,kwani kunahaja ya kushinikiza kila kona
mpaka taarifa hii isomwe kwenye Bunge ili ukweli ugundulike,
Hakuna maoni
Chapisha Maoni