KAMISHNA KOVA NI NOMA AZIKIDI KUYAMALIZA MAJAMBAZI,SASA KILA KUKICHA ANAYAKAMATA,SOMA HAPO KUJUA KWANINI
PICHANI NI KAMISHNA WA KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM KAMISHNA SULEIMAN KOVA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI |
Na Karoli
Vinsent
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam, limewakamataa
majambazi wawili kwa kosa la kumiliki silaha kinyume cha sheria na kuitumia
katika matukio ya ujambazi na kuwaletea Adha wakazi wa jiji hili.
Akithibitisha
kuyakamata majambazi hayo sugu,Kamanda wa kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishna
Suleiman Kova wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es
Salaam,ambapo alisema Kabla ya kukamata kwa bunduki hiyo watuhumiwa walikuwa
wamepanga kufanya tukio la ujambazi katika maduka ya MPESA na TIGO PESA
yaliyopo maeneo ya Sinza Madukani. Majambazi hao waliahirisha kufanya tukio
baada ya kushtukia mtego wa polisi.
Kamishna Kova alizidi kusema Mnamo
tarehe 10/09/2014 majambazi hao walikamatwa baada ya Polisi kupata taarifa kuwa
yamejipanga kufanya tukio la uhalifu maeneo ya YOMBO DOVYA na kisha kuweka
mtego katika nyumba ya ASIA D/O ALLY KASHINDE anayekadiriwa kuwa na umri wa
miaka 70 iliyopo maeneo ya Yombo Makangarawe (M) wa Kipolisi wa Temeke.
Baada ya kuwakamata
majambazi hao walipekuliwa katika chumba wanacholala ndipo ilipopatikana silaha
aina ya SMG yenye namba IC 5740 ikiwa na risasi 07 ndani ya magazine. Bunduki hiyo imekatwa mtutu na kitako.
Watuhumiwa wanaendelea kuhojiwa ili kuwezesha kuwakamata wengine
wanaoshirikiana katika genge hili la ujambazi
Kamishna Kova
aliwataja kwa Majina Majambazi hao ni KHAMIS
S/O AMBA, Miaka 40, Mkazi wa Yombo Makangarawe na OMAR S/O KHAMIS, Miaka 43,
Mkazi wa Masasi Nyasa Mtwara
Katika hatua
Nyingine jeshi hilo kanda Maalum ya Dar Es Salaam limejipanga kupambana na
Mitandao ya kijamii inayoandika na kuweka picha za Matusi kwa kusema Jeshi hilo
la polisi linashikiriana na Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) kuwabaini
wamiliki wa mitandao hiyo na kuwachukulia hatua kali za kisheria.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni