HABARI ILIYOTIKISA JIJI--KAULI MBOWE YAMTESA IGP MANGU,AIBUKA KUAPA KULA SAHANI MOJA NA MBOWE,SOMA HAPA KUJUA ZAIDI
PICHANI NI MWENYEKITI WA CHADEMA FREEMAN MBOWE PICHA NA MAKTABA
PICHANI Mkuu wa jeshi la polisi Nchini IGP Ernest Mangu
Na Karoli
Vinsent
SIKU moja kupita baada ya Mwenyekiti wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe,kutangaza mgomo na Maandamano
nchi nzima kwa ajili ya kushinikiza Bunge la Katiba lisitishwe mara moja kwa
madai Bunge hilo limeshindwa kutengeneza katiba ya Nchi, badala yake linatunga
Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM,
Naye Mkuu wa jeshi la polisi Nchini
IGP Ernest Mangu ameibuka na Kumvaa Mwenyekiti huyo wa Chadema Freeman Mbowe na
kusema Jeshi hilo halitakaubali kuruhusu Maandamano hayo kwani yanalengo ya
kuvuruga Amani ya nchi.
Kwani
Maandamano hayo pamoja na Migomo ni kinyume Cha sheria na kanuni
zinazosimamia Jamii kutii sheria na
utaratibu wake.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es
Salaam Kamishina wa polisi Oparesheni na Mafunzo Paul Chagonja -CP kwa Niaba ya
Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Ernest Mangu wakati wa Mkutano na Waandishi
wa habari kuzungumzia kauli aliyoitoa Kiongozi huyo wa Chadema,ambapo Chagonja
alisema Jeshi hilo halitakubali kushuhudia Migomo na Maandamo yenye kulenga
kuvuruga Amani
“Jeshi la
polisi tumepokea kwa masikitiko makubwa kauli aliyoitoa Freeman Mbowe kwamba
yeye pamoja na wafuasi wake wa chama chake wanajipanga kufanya maandamano na
migomo isiyokomo nchi nzima bila kufuata sheria,kanuni na taratibu za nchi ili
kushinikiza Bunge la katiba kuhailishwa ,sisi jeshi la polisi tunaonya vikali
kauli hiyo ambayo ni kinyume cha taratibu za nchi na hatutakubali”alisema CP-Chagonja
Chagonja alizidi kusema ieleweke wazi kwamba
siasa zina mipaka na zinapovuka mipaka
hiyo na kuanza kwenda kinyume cha sheria,kanuni na taratibu za nchi hiyo inageuka kuwa jinai na wala siyo siasa
tena.
Aidha
Chagonja alisema Jeshi hilo la polisi aliweza kumvumilia mtu yeyote
atakayetumia mwavuri wa siasa kutaka kuvuruga Amani na utulivu uliopo hapa
nchini na Jeshi halitasita kumchukulia hatua kali kama mhalifu Mwengine yeyote.
Katika
hatua nyingine Jeshi limewataka Wananchi wote kufuata sheria na taratibu za
nchi na kuepuka kauli zenye kulenga kuvuruga Amani ya nchi.
Kauli
hiyo ya Jeshi la Polisi nchini limekuja siku moja baada ya Mwenyekiti wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Freeman Mbowe kutangaza kuwepo kwa maandamano
bila kikomo nchi nzima kushinikiza kusitishwa kwa Bunge la Katiba aliloliita la
kifisadi linaloendelea mjini Dodoma.
Pia, Chama chake
kimeazimia kusimamisha mgombea mmoja katika nafasi ya urais ifikapo mwakani,
lengo likiwa kuung’oa utawala wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), uliowafanya
watanzania kuwa maskini wa kutupwa.
Akihutubia
mkutano mkuu wa uchaguzi, Mwenyekiti huyo wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe,
alisema umefika wakati sasa wa kuacha kukaa na kuzungumza na kwani
kinachoendelea Dodoma ni wizi na ukatili wa hali ya juu kwa wananchi wanyonge
ambao ndio walipa kodi.
“Samahani maneno
yangu ni makali na wala hapa sifanyi uchochezi…kinachoendelea Dodoma ni ufisadi
na wizi, tumekaa Kinana, tumekaa na Mangula, tumekaa na Rais Kikwete
tumekubaliana bunge lisitishwe lakini wanamwacha Sita afanye anachotaka kama
utafikiri ndiye Rais…
“Anachakachua
rasimu, anabadili kanuni, anavunja sheria anakusanya maoni utafikiri yeye ni
Warioba…hiki hakivumiliki, naomba mkutano huu utoke na tamko,” alisema Mbowe na
kushangiliwa na wajumbe wakiafiki.
Mbowe
akipendekeza maadhimio, alisema kinachotakiwa ni kuungana na kufanya maamuzi ya
kuandamana nchi nzima kushinikiza kusimamishwa kwa Bunge la Katiba
linaloendelea mjini Dodoma ambalo linafuja fedha za wanyonge ili hali katiba
haitapatikana
Hakuna maoni
Chapisha Maoni