SAKATA LA WANAFUNZI KUKOSA MIKOPO,TAHLISO YASEMA MAZITOSOMA HAPA KUJUA ZAIDI
PICHANI NI Mwenyekiti wa TAHLISO, JUMUIYA ya Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu (TAHLISO(Picha na Maktaba) |
Na Shehe
Semtawa
JUMUIYA ya Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu
ya Juu (TAHLISO), imesema ifikapo Oktoba, haitakuwa tayari kusikia kuna
mwanafunzi amekosa fedha za ada kwa kuwa serikali haina fedha.
Akizungumza na
wandishi wa habari jijjini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki Mwenyekiti wa
TAHLISO, Musa Mdede alisema ni aibu kwa wanafunzi kukosa fedha huku serikali
ikiendelea kuwalipa posho wajumbe
wa Bunge la Katiba.
Alisema uongozi
wa jumuiya hiyo umetoa msimamo huo baada ya kubaini kuwa fedha nyingi zinapotea
kwenye bunge hilo ambalo vikao vyake ni sawa na kupoteza muda.
“Tunaelekea
Oktoba, vyuo vyote vya elimu ya juu vinaelekea kufunguliwa, wanafunzi
wanatakiwa kuwa na fedha za kujikimu na ada… lakini kwa upuuzi unaondelea
Dodoma, TAHLISO hatitakubali kusikia Hazina hakuna fedha za kuwapa wanafunzi,”
alisema.Alisisitiza kwamba wana jumuiya hiyo wataandamana endapo serikali
itashindwa kuwalipa fedha hizo kwa wakati.
Kamishna wa
TAHLISO Kanda ya Mashariki, Elihuruma Himida aliitaka serikali kuwapatia mkopo
wanafunzi wote 58,037 waliomba.
‘Hatukubaliani
na uamuzi wa serikali wakuwapatia mkopo wanafunzi 30,000 pekee huku wengine
28,037 wakikosa… sisi tunaitaka iwapatie wanafunzi wote wanaostahili tena kwa
wakati, hili la kusema haina fedha ni ubabaishaji tu,” alisema Himida.
Himida, alisema
mwaka 2010 serikali ilipandisha kiwango cha fedha ya kujikimu kutoka sh 5,000
hadi sh 7,500 kutokana na kuongezeka kwa gharama za maisha fedha hizo hazitoshi
hivyo ni vema wakaongeza na kuwa sh 15,000 kwa siku
Hakuna maoni
Chapisha Maoni