HABARI ILIYOTIKISA JIJI--MBOWE NI KIBOKO ASIMAMISHA JIJI LA DAR KWA SAA TANO,POLISI WAHAHA KUTULIZA NGUVU YA UMMA,HABARI KAMILI SOMA HAPA
Na Karoli
Vinsent
KATIKA hali
isiyokuwa ya Kawaida Jeshi la polisi Makao Makuu,limeonja Joto la Jiwe kutoka
kwa Wanachama pamoja na wapenzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Chadema,pale walipojitokeza kwa wingi kwenda kumsindikiza Mwenyekiti wa Chama
Hicho Freeman Mbowe kwenda kuonana na Jeshi la Polisi kuhusu maandamano
aliyoyatangaza.
TUNDU LISSU KUSHOTO KATIKATI MBUNGE JOHN MNYIKA MWISHO KULIA GWIJI LA SHERIA NCHINI MABELE MARANDU WAKIWASILI KWENDA KUMWOKOA MBOWE |
Mwandishi wa Mtandao huu alifikia
Makao Makuu ya Jeshi la Polisi nchini Jijini Dar Es Salaam majira ya nne
asubuhi na kukuta umati mkubwa wa watu ukiwa ikimsubili Mbowe huku Jeshi la
polisi likijizatiti kuhimalisha ulinzi katika maeneo hayo kwa kutumia mpaka
Mpwa,magari ya kumwaga Machozi.
Ilipofika Saa tano asubuhi Mwenyekiti
Taifa wa Chama hicho Freeman Mbowe aliwasili huku akisindikizwa na Magwiji wa
Sheria kutoka ndani ya chama hicho akiwemo,Tundu Lissu,Profesa Abdala
Safari,Mabele Marandu, Peter Kibatala na wakaingia moja kwa moja kwenda kwenye
ofisi za Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini huku wakishangiliwa na wananchama wa Chama
hicho,
TUNDU LISSU AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI BAADA YA KUMALIZIKA MAHOJIANO NA JESHI LA POLISI |
Mbowe
pamoja na magwiji hao washeria waliruhusiwa kuingia huku Jeshi la polisi
likiwazuia mtu mwengine kuingia ofisi hapo na shughuli zikisimama,
Ilipofika majira ya Saa sita mchana Waandishi
wa Habari kutoka Vyombo tofauti nchini wakiwa wakisubili nje kujua hatma ya
kesi hiyo,ndipo Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa Gazeti la Tanzania Daima
Josephati Issango alikumbana na adha baada ya polisi kumletea shida huku polisi
wakisahau mwandishi huyo anafanyamajukumu yake ya kazi ndipo waandishi wengine
wakaende kumsaidia,
Baada ya kufika saa tisa kamili jioni
Mwanasheria Mkuu wa Chama cha demokrasia na Maendeleo Chadema Tundu Lissu
alitoka huku akiambana na wanasheria wenzake akiwemo Mabele Marandu,Profesa
Safari,Kibatala wakenda moja kwa moja kwa waandishi wa habari kueleza hali
halisi.
Ambapo Tundu Lissu Alisema Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe
amekutwa na hatia kutokana na Maongezi yake aliyoyatoa siku ya Jumapili wakati
wa mkutano mkuu wa chama hicho,na kusema kwa sasa kazi iliyobakia ni kumwekea
Dhamana,
PICHANI KUSHOTO NI MKURUGENZI WA ORIGANIZASHENI WA CHAM HICHO BENSON KAGAILA KULIA NI JOHN MNYIKA WAKIFAFAUNUA JAMBO |
“Kwanza nawatoa hofu wanachama wenzangu
kwamba Mwenyekiti wetu yuko salama,na sasa amekutwa na hatia sasa kilichobaki
sahivi ni kupatiwa Dhamana,na huku nilipomwacha anakamilisha taribu zote za Dhamana
ili apatiwe dhamana yenyewe,”Alisema Lissu,
Tundu Lissu,ambaye ni Mbunge wa
Singida Mashariki Chadema aliwataka wanachama wa Chama hicho kuondoka taratibu
maeneo hayo na kuacha kuondoka kwa makundi kwani kufanya kutalifanya Jeshi la
Polisi kufuta Dhamana ya Mbowe.
“Jeshi la Polisi limewaomba wanachama
wote wachadema mliokuwa hapa kuondoka bila makundi yeyote,kwani tusipofanya
Hivyo Jeshi la polisi limesema litaifuta Dhamana yenyewe na Kumweka
ndani,kwahiyo nawataka tuondoke kimya kimya bila makundi,kwani atutaki kuhalibu
sifa ya yetu kwenye uchaguzi wa Mwezi Desemba “Alizidi kusema Gwiji huyo wa
Sheria kutoka Chadema huku akishangiliwa na wanachama wa Chama hicho,
Naye Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama hicho
pia ni Mwanasheria aliyobobea kutoka Mahakama kuu Mabele Marandu aliumbia
Mtandao huu kwamba yeye pamoja na wanasheria wengine watapambana kwa hali na
mali kuhakikisha wanamwokoa mwenyekiti wa chama hicho.
“Sikiliza
mwandishi mimi ni Mwanasheri niliyobobea nitapambana na wenzangu kuhakikisha
tunamwokoa mwenyekiti wetu mengine siwezi kuzungumza”alisema Marandu
Hakuna maoni
Chapisha Maoni