HIVI NDIVYO JESHI LA POLISI LIKIMSHUSHIA KIPIGO MWANDISHI MWANDAMIZI WA GAZETI LA TANZANIA DAIMA JOSEPHATI ISSANGO,PASIPOKUWA NA KOSA LOLOTE,
Na Karoli
Vinsent
SIKU moja
kupita Baada ya Makamu wa Rais Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal kuvitaka Vyombo vya
ulinzi kufanya kazi kwa ukaribu na Waandishi wa Habari,lakini sasa Jeshi la
polisi limeipuuzia kauli hiyo na kuzidi kuwafanyia unyama waandishi wa Habari.
Hayo yameonekana Leo
Jijini Dar es Salaam wakati waandishi wa Habari walipokuwa wakichukua taarifa
za Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman Mbowe
alipokuwa polisi Makao makuu,
Ambapo Polisi walikuwa
wakilinda ulinzi maeneo hayo walikuwa wakiwazuia waandishi na kuwafanyia unyama
wa hali ya Juu ikiwemo kuwapiga hadi kuwapelekea maumivu katika sehemu
mbalimbali za mwili.
Akizungumza na Mwandishi
wa Mtandao huu juu ya Unyama aliofanyiwa na jeshi la Polisi Mwandishi
Mwandamizi wa Gazeti la Tanzania Daima Josephati Issango alisema anasikitika
sana kwa Jeshi la polisi kumfanyia unyama huo huku wakijua yeye ni mwandishi.
“hivi Jeshi la Polisi
tumelikosea nini maana mimi hapa na peni na kitabu tu nachukua taarifa sasa leo wananifuata na kunipiga tena wanivunja mguu,na
kunipora vifaa vyangu nilivyonavyo kwa kosa lipi wakati kazi yangu mimi ni
kuchukua taarifa tu”alisema Issango
|
Hakuna maoni
Chapisha Maoni