UTAFITI--MKOA WA ILALA UNAONGOZA KWA VITENDO VYA UBAKAJI,SOMA HAPA KUJUA UTAFITI WA TAMWA
PICHANI NI Kaimu Katibu Mkurugenzi wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Gladnes Munuo |
Na Karoli
vinsent
KILA siku wastani wa watoto watano
wananajisiwa katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Kaimu Katibu Mkurugenzi wa Chama cha
Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Gladnes Munuo alisema hayo jijini hapa
jana wakati wa uzinduzi wa ripoti ya pili ya utafiti kuhusu unyanyasaji na
ukatili wa kijinsia.
Alisema kwa mujibu wa Mganga Mkuu
wa Manispaa ya Ilala, Willy Sangu ubakaji ulipungua mwaka 2013 lakini katika
robo ya kwanza ya mwaka 2014 uliongezeka ambapo idadi ya waliohudumiwa katika
hospitali ya Amana baada ya kufanyiwa ukatili wa kijinsia ni 310.
Alisema kwa mujibu wa Ofisa
Ustawi wa Jamii wa Kituo cha ‘One Stop Centre’ kilichopo katika hospitali hiyo,
Eva Mbilinyi vitendo vya ubakaji vipo kwa kiwango cha juu hali inayodhihirishwa
na takwimu za wanaohudumiwa katika kituo hicho.
Alisema tangu kituo hicho
kizinduliwe mwaka jana kimepokea matukio 253 ya unyanyasaji wa kijinsia ambapo
kesi 35 zilifikishwa mahakamani hadi Juni 10.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni