BODI YA MIKOPO ELIMU YA JUU HOI KIFEDHA,WAZIRI KAWAMBA AJIKANA NA KUIBEBESHA MZIGO WA LAWAMA BODI SOMA HAPA KUJUA ZAIDI
Na Karoli Vinsent
BODI ya Mikopo ya Elimu ya Juu
(HESLB) hiko katika hali mbaya ya Kifedha ambayo imepelekea wanafunzi 28,037 kati ya
wanafunzi wote 58,037 waliomba katika mwaka 2014-2015 kukosa mkopo,kutokana
na Bodi hiyo kushindwa kukusanya Fedha.
Hayo yamesemwa leo
Jijini Dar es Salaam na, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Shukuru
Kawabwa wakati akizindua Bodi Mpya ya Watendaji wa Bodi ya Mkopo nchini,ambapo
Mbali na Kuizindua Bodi hiyo Waziri huyo alisikitishwa kwa Bodi hiyo kushindwa
kukusanya fedha kutoka kwa wanafunzi wanaomaliza vyuo Vikuu Nchini kwani kushindwa kufanya hivyo kumepelekea Bodi kuwa
katika hali mbaya Kifedha.
“Yaani hili ni jambo
la Kushangaza Bodi ya Mikopo ina zaidi ya miaka tisa imeshindwa hata kuwatambua
watu inayowadai,na sijui kwanini, maana mnashindwa kutambua kiini cha haya
matatizo,maana mwaka jana kwenye makusanyo yenu mmekusanya Bilioni 7 tu,harafu
mwaka huo huo mmepewa pesa zaidi ya Bilioni 300,kwa mfumo huu ndio mnapelekea
wanafunzi kukosa mikopo”alisema Kawabwa
Waziri
Kawabwa alizidi kusema Bodi hiyo imekuwa ikifanya kazi kitaratibu sana kutokana
na kushindwa hata kuwashawishi makampuni binasfsi ikiwemo Banki mbalimbali
katika kuwakopesha wanafunzi masikini nchini na kuwataka kutafutafuta ufumbuzi
wa tatizo hilo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Bodi hiyo
Mpya ya Mkopo Dokta Charles Kimei
alisikiti kwa utendaji kazi wa Bodi na kusema kwa mfumo huo hakuna hata sekta
binafsi hususani mabanki watakaoikopesha Bodi hiyo.
“Mimi nashukuru sana kuchaguliwa kwenye Bodi hii mpya ya wakurugenzi wa
Bodi ya Mkopo nchini ila changamoto za Bodi ya Mkopo ni kubwa sana
nakuhakikishia Waziri nitazishughulikia hususani kwenye makusanyo kutoka kwa
wanafunzi wanapomaliza Vyuo Vikuu,harafu hata hili la Mabanki kushindwa
kuikopesha bodi hii inatokana ubovu katika ukusanyaji Fedha yaani unakusanya asilimia
7 tu kwa mwaka unatamshawishi Banki gani ije kukopesha Bodi hii”alihoji Kimei.
Kazinduliwa kwa Bodi hii mpya kunazidisha
maswali kutoka kwa Jamii kutokana na Bodi hiyo kutangaza Rasmi kwamba Wanafunzi
28,037 kati ya wanafunzi wote 58,037
waliomba katika mwaka 2014-2015 kukosa mkopo,
Kauli hiyo ya Bodi ya
Mkopo ndio ikawafanya JUMUIYA ya
Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu (TAHLISO), Kusema ifikapo Oktoba, haitakuwa
tayari kusikia kuna mwanafunzi amekosa fedha za ada kwa kuwa serikali haina
fedha.
Akizungumza na wandishi wa habari jijjini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki
Mwenyekiti wa TAHLISO, Musa Mdede alisema ni aibu kwa wanafunzi kukosa fedha
huku serikali ikiendelea kuwalipa posho
wajumbe wa
Bunge la Katiba.
Alisema
uongozi wa jumuiya hiyo umetoa msimamo huo baada ya kubaini kuwa fedha nyingi
zinapotea kwenye bunge hilo ambalo vikao vyake ni sawa na kupoteza muda.
“Tunaelekea Oktoba, vyuo vyote vya elimu ya juu vinaelekea kufunguliwa,
wanafunzi wanatakiwa kuwa na fedha za kujikimu na ada… lakini kwa upuuzi
unaondelea Dodoma, TAHLISO hatitakubali kusikia Hazina hakuna fedha za kuwapa
wanafunzi,” alisema.Alisisitiza kwamba wana jumuiya hiyo wataandamana endapo
serikali itashindwa kuwalipa fedha hizo kwa wakati.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni