Zinazobamba

MADUDU YA LOWASSA YAZIDI KUFICHUKA,PICHA YAKE YAZIDI KUIBUA MAMBO SOMA HAPA ZAIDI

                           
WIKI Mbili zilizopita kulikuwa na mjadala mkali sana kwenye kikao cha uhariri(gazeti la mwananchi) cha kuamua habari kuu za gazeti. Mjadala ulikuwa juu ya picha iliyotumwa na mpiga picha wetu kutoka
          Dodoma. Kuna baadhi ya wenzetu walitaka picha hiyo iwekwe ukurasa wa mbele wa gazeti. Kuna wengine hawakutaka kabisa iwekwe gazetini kwani gazeti lingeonekana ni nyenzo ya propaganda za siasa za Urais ndani ya CCM. Muafaka ukafikiwa kwamba iwekwe nyuma kwenye ukurasa wa michezo, ingawa nako kulikuwa na mjadala kwamba Lowasa ni mwanamichezo tangu lini. Wengine wakahoji kwamba tukiulizwa kwamba ilikuwaje gazeti letu likawa kwenye mazoezi ya Lowassa tutasemaje
           kwani huwa hakuna taarifa kwa umma kuhusu lini Lowasa anafanya mazoezi na anapitia njia zipi.
Baada ya mzozo kuisha, baadhi yetu tukaamua kufanya uchunguzi wa kina kwamba ilikuwaje mpiga picha wa gazeti akawa sehemu ya mazoezi ya Lowasa? Je alialikwa? Je alikutana naye kwa bahati
mbaya? Pia wakati tunajadili kuhusu hii picha, kulikuwa na presha kubwa sana kutoka Kwa Mzee Lowasa mwenyewe kuja kwa viongozi wetu wakuu kwamba kwa gharama yoyote ile (wengine walisema
          milioni 10) picha hiyo lazima itoke ukurasa wa mbele. Bahati nzuri mantiki ikashinda na tukaliokoa gazeti kutoka kwenye aibu ambayo tungeipata. Katika uchunguzi wetu ilibainika kwamba Bwana Abubakari
Liongo, mbeba hela za Lowasa kwa waandishi, aliwatafuta wapiga picha wetu na kuwaambia kwamba kuna tukio muhimu la dakika 10 kwa Lowassa. Akatuma gari kumpeleka mpiga picha alipokuwa anatembea Mzee. Akapiga picha ya kutembea.
           Washauri wa  Mzee wakamuomba akimbie kidogo, ikapigwa picha ya kukimbia. Mpiga picha akaambiwa arudishwe lakini akaamua kubaki kwakuwa ilikuwa ni karibu na mahali anapoenda. Akashuhudia Mzee akipanda gari na kuondoka. Ukitazama
            picha kwa makini utaona Landcruiser iko kwa nyuma. Swali ni kwanini hadaa yote hii? Sababu ni kwamba ni kweli afya ya Mzee Lowassa imedhoofika. Kila mwezi anaenda kutibiwa Ujerumani, mikono inatetemeka na jicho moja linakaribia kufunga kabisa. Sababu ya kutaka picha hii itoke kwa gharama kubwa ni kujaribu kuuonyesha umma kwamba yeye ni mzima. Wapi wazee wengi wanaofanya mazoezi kila siku lakini hawahangaiki na kupigwa picha. Mzee Mwinyi ana miaka 89 na anatembea na kukimbia kila siku.
        Dr. Salim anakimbia kila siku. Jenerali Mirisho Sarakikya ana miaka 80 na anapanda Mlima Kilimanjaro kila mwaka kwa mwaka wa 30 sasa. Hatuoni wakihaha kupiga picha na kuzisambaza mitandaoni. Mazoezi magumu kwa Lowasa ni kushika kikombe cha chai kwa dakika 3.


Binafsi nimepata woga. Nimepata woga kutokana na uroho mkubwa wa madaraka ulioonyeshwa na timu ya Lowassa. Wako tayari kufanya chochote kupata madaraka. Bahati nzuri hadi sasa mambo mengi wanayoyafanya ni maigizo tu, ikiwemo hili la kutengeneza mazoezi feki na kuitengea bajeti picha ili ichapwe gazetini ni kusambazwa mitandaoni. Mungu Ibariki nchi yetu.

Hakuna maoni