HABARI KUBWA LEO--UKAWA WALIA NA UGEUGEU WA RAIS KIKWETE KWENYE MISIMAMO,MBOWE ADONDOSHA CHOZI,SOMA HAPA KUJA ZAIDI
UKAWA |
Na Karoli
Vinsent
LICHA ya
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta kujinadi kwamba Thelusi 2 ya
wajumbe inapatikana wakati wa upigaji kura kuipitisha rasimu iliyopendekezwa na Bunge hilo, kwa madai
wajumbe Bungeni hapo wasiokuwepo watatumia hata njia ya Fax,simu pamoja na “Internet”
mtandao kupiga kura,
Nao Viongozi Umoja wa Kutetea Katiba
ya Wananchi UKAWA umemjia juu Rais Jakaya Kikwete kwa kitendo chake cha
Kumwacha mwenyekiti wa Bunge hilo Samwel Sitta kwa kuendelea kufanya hujuma kwa
watanzania kwenye mchakato wa katiba,
Kwani Duniani kote hakuna kura
yeyote inayopigwa kwa njia ya simu wala Internet na anavyofanya hivyo samweli
sitta ni kutaka kufanya mambo pasipo kisheria,
Hayo yamesemwa mda huu Jijini Dar es
Salaam na Viongozi wa vyama vikuu vya
upinzani nchini wanaounda Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA wakati wa
Mkutano na Waandishi wa Habari,ambapo Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF
Profesa Ibrahim Lipumba alimshangaa Rais Jakaya Kikwete kwa kuyakimbia matatizo
nchi na kwenda nje ya nchi na kushindwa kuliokoa taifa katika hujuma anayofanya Samwel sitta.
“Rais Kikwete amekuwa mtu wa kwenda
Marekani kila wakati yanapotokea Matatizo,na leo anamwacha Samwel Sitta anafanya
mambo ya ajabu, ambayo duniani hayajawai kutokea kura kwa njia ya simu,harafu
Rais Kikwete anashindwa kukemea uragai huu,hivi huyo ni kiongozi gani”Alihoji
Profesa Lipumba
Profesa Lipumba ambaye ni Gwiji la
masuala Uchumi kimataifa alizidi kuzungumza kwa Uchungu ambapo alimshangaa Rais
Jakaya Kikwete kuonyesha ugeugeu kwa watanzania kwani wakati wa Mkutano kati
yake na Vyama vya kisiasa nchini vilivyo chini ya Kituo cha Demokrasia nchini (
TCD).
Katika mkutano huo Rais Kikwete
alikubali wazi kwamba bunge Maalum la sasa aliwezi kuleta katiba cha kushangaza
leo ameshindwa hata kuingilia kati utoto
unaofanywa na Samwel Sitta kwa Watanzania.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Chama cha
demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman Mbowe naye pia alimshangaa Rais Jakaya
kikwete kushindwa kuongoza nchi na kukimbilia Marekani na kumwachia Samweli
sitta ndio kiongozi wa nchi na kufanya mambo ya hovyo katika Bunge la Katiba.
“Rais kikwete amekosa hata utashi
kuliokoa Bunge hili, yeye analikimbia Tatizo anakwenda Marekani,yaani leo Sitta
anakuwa na Sauti kuliko Kikwete,jamani watanzania wenzangu nchi hii haina
kiongozi huyo, ndio kiongozi kweli leo anashindwa hata kuwaonea huruma
watanzania wanavyolia na Umasikini,leo mapesa yanapotea hivi”alisema Mbowe,
Aidha Mbowe alizidi kutoa masikitiko
yake kwa Rais kikwete kwa kuonyesha wazi kwamba ni watu wakubadilika badilika
na kushindwa kusimama kwenye msimamo sahihi na wenye tija kwa manufaa kwa
taifa,kutoka na kushindwa kusimamia maazimio aliyoyatoa Kwenye mkutano kati yake
na Vyama vya Kisiasa
“Jamani
nataka mumfahamu Rasi Kikwete alivyo,wakati wa kutano baina yangu na yeye au
Viongozi wa Vyama vya Kisiasa ambao waliokuwepo hadi viongozi CCM Kinana na
Mangura,katika Mkutano huo anakubali wazi katiba haiwezi kupatikana na Bunge
hili na tena tunakubaliana wote mchakato uendelee baada ya uchaguzi mkuu,sasa
inakuwaje leo wakina sitta wamekuwa wanaipinga kauli yake hivi Rais unakuwa
Kimya kiasi hichi na kukimbilia Marekani,kwa mfumo nawaomba watanzania wajipime”alisema
Mbowe
Kuhusu
hukumu ya Kesi iliyofungiliwa na Mwandishi wa Habari Mwandamizi Saed Kubenea Katika kesi hiyo, Kubenea aliyekuwa
akiwakilishwa na mawakili, Peter Kibatara na Mabere Marando, anaitaka Mahakama
Kuu itoe tafsiri sahihi juu ya mamlaka ya Bunge Maalum la Katiba, chini ya
kifungu cha 25 (1) na (2) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 ya
mwaka 2011 na Mahakama hiyo kutoa hukumu Maoni ya wananchi yaheshimiwe na
kusema hayo mengine mahakama hayawezi kuyatolea ufafanuzi kwa madai ni
yakisiasa,
Mwanasheria Mkuu wa Umoja wa
Kutetea katiba ya Wananchi Tundu Lissu aliishangaa Mahakamu kuu kugundua Bunge
la Maalum la Katiba kwamba limefanya Makosa kuzika maoni ya yaliyotolewa na
Jaji Warioba na kushindwa kuchukua hatua badala yake Mahakama hiyo imeishia tu
kusema suala hilo ni la kisiasa kwani kufanya hivyo kuzidisha mashaka kwa
mahakama kuu,
Kuhusu maandamano na mikutano ya Ukawa
kukataliwa na Jeshi la Polisi nchini.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe alisikitika kwa Jeshi la Polisi kuwanyima haki
ya Msingi Kikatiba ya Kufanya Maandamoni kwani yeye anashangaa Jeshi hilo
kukiruhusu chama cha Mapinduzi CCM kiendelee kufanya Mikutano yao huku
kikiwakataza Chadema,CUF,wasifanye mikutano.
“Kiongozi
wa Afrika ya Kusini Mzee Nelson Mandela alisema Serikali yeyeto inayotumia
Mabavu kuwanyima haki wananchi basi wananchi watachoka watatafuta njai nyingine
kudai haki,kiukweli leo Chadema tukitaka hata kufanya mikutano majimboni kwetu
tunakataliwa na jeshi la polisi,lakini Kinana anaruhisiwa kuendelea kujinadi
kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa sisi tunakatazwa ,mimi mwenyewe nilitaka
kwenda Jimboni kwangu nimezuliwa na polisi jamani haki za msingi tunanyimwa”alisema Mbowe.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni